Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Serikali yamnyang’anya mzawa mradi wa bomba
Serikali yamnyang’anya mzawa mradi wa bomba
By Habari Tanzania | Published  02/27/2007 | Habari za Kitaifa | Rating:
na Nasra Abdallah

SERIKALI imetangaza rasmi kumnyang’anya mwekezaji wa ndani, Kampuni ya Africommerce, mradi mkubwa wa kujenga mabomba ya kusafirisha mafuta.

Pia imeionya kampuni hiyo kuacha kuitisha serikali kupitia vyombo vya habari, kwa sababu haitishwi wala kuyumbishwa na mtu yeyote katika kutekeleza azma yake ya kuwaletea wananchi maendeleo.

Uamuzi huo wa serikali ulitangazwa jana na Waziri wa Mipango, Uchumi na Uwezeshaji, Dk. Juma Ngasongwa, wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, Dar es Salaam.

Alisema serikali imeamua kuipa Kampuni ya Noor Oil and Industrial Technology Ltd (NOIT) mradi huo, baada ya kuridhika na mapendekezo yake ya awali ya kuwekeza kiasi cha dola za Marekani bilioni 2.6 katika mradi huo.

“NOIT ina uwezo wa kujenga kiwanda kikubwa cha kusafisha mafuta ghafi na kutandaza mabomba ya kusafirisha mafuta kutoka Dar es Salaam hadi jijini Mwanza.

“Iwapo kiwanda hicho kitajengwa kitakuwa cha pili kwa ukubwa barani Afrika na uzalishaji wake unakadiriwa kuwa mapipa 120,000 hadi 200,000 kwa siku, kiwango ambacho ni kikubwa ikilinganishwa na matumzi ya Tanzania ambayo hutumia mapipa 30,000 kwa siku,” alisema Ngasongwa.

Waziri huyo aliwaita waandishi wa habari ofisini kwake kutoa tamko la serikali kuhusu madai ya Kampuni ya Africommerce, ya kuipa siku 30 kutizama upya uamuzi wake wa kuinyang’anya mradi huo, vinginevyo iwe tayari kuburuzwa mahakamani.

Akizungumza kuhusu mradi huo na vitisho vya Mkurugenzi wa Africommerce, Elisante Muro, Waziri Ngasongwa alisema mradi ambao awali ilipewa kampuni hiyo, ni wa kusafirisha mafuta ghafi na kutandaza mabomba ya kusafirisha mafuta kutoka jijini Dar es Salaam hadi jijini Mwanza.

Alisema kati ya Februari 20 na 21, mwaka huu, Muro alitoa malalamiko kupitia vyombo vya habari na kutishia kuishitaki serikali kwa hatua yake ya kuipa Kampuni ya NOIT mradi huo kinyume cha makubaliano ya awali yaliyokuwa yamefikiwa kati yake na serikali.

Alivitaja vitisho hivyo kuwa, ni pamoja na kuitaka serikali iendelee kutambua kuwa mradi huo ni wa Africommerce pamoja na kuipa siku 90 ili kutazama upya uamuzi wake kabla ya kuiburuza mahakamani.

Waziri Ngasongwa alisema madai ya kampuni hiyo yanalenga kuueleza umma kuwa serikali imepora mradi huo na kwamba haiwajali wawekezaji wazalendo, inawavunja nguvu na haiwapi ushirikiano wa kuendeleza miradi yao.

“Kwa mujibu wa katiba ya nchi yetu, mtu yeyote anayo haki ya kufikisha madai yake mahakamani pale atakapoona hajatendewa haki, hali kadhalika, serikali ina haki ya kujitetea pale itakapokuwa imeshtakiwa mahakamani.

“Kutokana na msingi huo wa kikatiba, kampuni ya Africommerce inayo haki ya kupeleka madai yake mahakamani ili haki itendeke,” alisema Waziri Ngasongwa

Alisema Africommerce imekaa na mradi huo kwa muda wa miaka 24 bila kubainisha kuwa haina uwezo wa kifedha wa kuutekeleza na kwamba madai inayoyatoa ya kukwamishwa na serikali ni visingizio visivyo na msingi wowote.

Waziri Ngasongwa alisema serikali isingeweza kuizuia kampuni hiyo, kujenga mradi huo kama ingekamilisha taratibu za kuuendesha, ikiwa ni pamoja na kuwa na uwezo wa kifedha na kitaalamu unaohitajika kwa miradi mikubwa.

“Ni dhahiri kuwa, kushindwa kwa Africommerce kutekeleza mradi huo tangu mwaka 1983, hakuwezi kutokana na njama za serikali bali ni uthibitisho wa uwezo wake mdogo,” alisisitiza Waziri Ngasongwa.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.