WAZIRI wa Sayansi, Teknolojia na Elimu ya Juu, Profesa Peter Msolla, juzi alishindwa kuwahutubia wanachuo wa Chuo Kikuu Huria (OUT) kituo cha Arusha kutokana na giza.
Prof. Msolla, ambaye alitarajiwa kufika chuoni hapo saa 9.30 alasiri, alichelewa, na badala yake alifika saa 12.00 jioni na kuanza kutembezwa katika maeneo mbalimbali ya chuo.
Baada ya kukagua eneo la chuo, alikwenda jukwaani kwa ajili ya kutoa hotuba kwa jumuiya ya wanachuo, ambayo hata hivyo alilazimika kuikatisha baada ya kushindwa kusoma kutokana na giza, licha ya kuwashwa kwa taa za gari dogo aina yaToyota, Land Cruiser ili aweze kuona vizuri..
Prof. Msolla pia hakupata muda wa kuulizwa maswali na wanajumuiya hao kama ilivyokuwa imepangwa.