Habari Tanzania - http://www.habaritanzania.com
Wakamatwa kwa mlipuko wa treni India
http://www.habaritanzania.com/articles/3134/1/Wakamatwa-kwa-mlipuko-wa-treni-India
By Habari Tanzania
Published on 02/25/2007
 
POLISI nchini India imesema inawashikilia watu watatu wanaodaiwa kuhusika na ulipuaji wa treni ya abiria ya Samjhauta (Friendship) Express) iliyokuwa ikitokea India kuelekea Pakistan.

DELHI
POLISI nchini India imesema inawashikilia watu watatu wanaodaiwa kuhusika na ulipuaji wa treni ya abiria ya Samjhauta (Friendship) Express) iliyokuwa ikitokea India kuelekea Pakistan.

Watu wasiopungua 68 Jumapili iliyopita walifariki dunia katika ajali ya moto iliyotokea katika treni hiyo, wengi wao wakiwa ni raia wa Pakistan

Wanaume wawili na mwanamke mmoja walikamatwa Kaskazini mwa Rajasthan kufuatia polisi wa nchi hiyo kupewa taarifa na msamaria mwema.

India ilisema itashirikiana na Pakistan katika kufanya uchunguzi wa kuwasaka watu walihusika katika mlipuko uliosababisha mauaji ya watu hao.

Polisi walisema watu hao walikamatwa katika Wilaya ya Bikaner mpakani mwa Pakistan na wilaya hiyo.

Polisi wanaendelea na uchunguzi na hakuna taarifa sahihi nani alihusika na shambulio hilo lililotokea kilometa 80 kutoka mji wa Delhi.

Hata hivyo polisi walitoa picha za watu wawili ambao walipanda katika treni hiyo muda mfupi kabla haijalipuliwa.