Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Serikali yashauriwa kubuni sera ya kilimo cha umwagiliaji
Serikali yashauriwa kubuni sera ya kilimo cha umwagiliaji
By Habari Tanzania | Published  02/25/2007 | Habari za Kitaifa | Unrated

Na Kizitto Noya, Bagamoyo

WADAU wa sekta ya kilimo nchini wameishauri serikali kuanzisha sera maalum ya kilimo cha umwagiliaji na kuisimamia vizuri ili kumwezesha mkulima mdogo na wa kati kushiriki kilimo hicho kwa maendeleo yake na taifa.

Aidha, wadau hao wameishauri serikali kuajiri maafisa umwagiliaji katika halmashauri zote za wilaya na manispaa kote nchini ambao watasaidia kuhakikisha kilimo hicho kinatekelezwa kikamilifu.

Wakizungumza katika warsha ya siku mbili ya kujadili sera na mkakati wa kitaifa wa kilimo cha umwagiliaji iliyofanyika mjini Bagamoyo, Mkoa wa Pwani wiki hii, wadau hao walisema kuwa kilimo ambacho ni uti wa mgongo wa Tanzania, kinatakiwa kuboreshwa ili kukidhi mahitaji ya watu na taifa.

Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Kanali Anatory Tarimo akichangia katika semina hiyo alisema kuwa ni aibu kwa nchi kama Tanzania kuendelea kukumbwa na janga la njaa katika baadhi ya mikoa yake wakati ina zaidi ya ekari 1milioni za ardhi inayofaa kwa kilimo cha umwagiliaji.

"Nadhani siyo busara kuzungumzia njaa ya ukame katika nchi kama Tanzania yenye mabonde mengi yanayofaa kwa kilimo cha umwagiliji. Badala yake, tunaishauri serikali iainishe sera ya umwagilijai ambayo itamwezesha mkulima kulima kwa wakati wakati wote wa mwaka kwa faida yake na taifa,"alisema Kanali Tarimo.

Naye Mkuu wa wilaya ya Ulanga, Mkoani Morogoro, Dk Rajab Rutengwe alitaka kuwe na utaratibu wa kuyabainisha maeneo yanayofaa kwa kilimo cha umwagiliaji na kuyadhibiti ili kuepusha migogoro ya ardhi baina ya wakulima na wafugaji.

Alisema ni wazi kuwa maeneo yanayofaa kwa kilimo cha umwagiliaji mara nyingi yamekuwa yakitumika kulishia mifugo na bila udhibiti wa maana katika maeneo hayo kuna uwezekano wa kuleta migogoro ya ardhi katika jamii.

Awali, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika, Mohammed Muya alisema serikali iko katika hatua za mwanzo za kuyandaa maeneo kwa ajili ya kuwakaribisha wawekezaji kuweka katika sekta ya kilimo.

"Tunawakaribisha wawekezaji wakubwa katika sekta ya kilimo waje kuwekeza katika kilimo cha umwagiliaji ili kuweza kuzalisha kulingana na mahitaji yetu," alisema.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.