Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Mwanasiasa adai wananchi walazimishwa kuchangia sekondari
Mwanasiasa adai wananchi walazimishwa kuchangia sekondari
By Habari Tanzania | Published  02/25/2007 | Habari za Kitaifa | Unrated

Na Muhibu Said

BAADHI ya viongozi wa serikali Wilayani Bariadi, mkoani Shinyanga wamedaiwa kuwalazimisha wananchi kuchangia ujenzi wa sekondari kwa kutishia kuuza mifugo yao na kung'oa mabati ya nyumba zao iwapo hawatachangia ujenzi huo.

Madai hayo yalitolewa jana na Mwenyekiti wa Chama cha United Democratic (UDP) ambaye pia ni Mbunge wa Bariadi Mashariki, John Cheyo, alipozungumza na waandishi wa habari, makao makuu ya chama hicho, jijini Dar es Salaam.

Alisema analaani kitendo hicho kwa kuwa suala la kuchangia ujenzi wa shule, ni la hiari.

Hata hivyo, alisema pamoja na hivyo, wananchi wilayani humo wameitikia wito wa serikali ambapo kwa kipindi cha mwaka 2006/2007, wamechangia ujenzi wa sekondari 45, hatua ambayo imeokoa zaidi ya Sh4 bilioni ambazo zingetolewa na serikali kwa ajili ya ujenzi wa shule hizo.

"Tuache tabia ya kusukuma wananchi kwa nguvu, kutishia kuchukua mali zao, tukienda na tabia hiyo, wananchi wataichukia serikali yao na itafanya viongozi wakose kura katika uchaguzi ujao kwa sababu badala ya suala hilo kuwa msaada itakuwa kero," alisema Cheyo.

Cheyo, alisema taarifa za kitendo hicho amezipata kutoka kwa baadhi ya wananchi wilayani humo ambao walimpigia simu na kumtolea mfano wa wananchi wa kijiji cha Ikunguilipu, kilichopo wilayani humo ambao waliamua kuchangia ujenzi wa shule kwa awamu, kwa kuanzia na shule ya kijiji, lakini wakavamiwa na viongozi hao na kuwalazimisha kujenga shule ya kata na maabara.

Hata hivyo, mwanasiasa huyo aliilaumu serikali ya awamu ya nne kwa kutenga bajeti ndogo katika sekta ya elimu na kuishauri kujenga utamaduni wa kuweka bayana mahitaji ya sekta hiyo ili wananchi waweze kujiandaa mapema kuchangia suala hilo.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.