Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Tanzania yahimiza matumizi rasimali Mto Nile
Tanzania yahimiza matumizi rasimali Mto Nile
By Habari Tanzania | Published  02/24/2007 | Habari za Kitaifa | Unrated

Na Mwandishi Wetu, Mwanza

SERIKALI imewahimiza raia wa nchini zilizomo kwenye Bonde la Mto Nile kulinda, kutumia vizuri na kuendeleza rasilimali zake kwa manufaa ya nchi hizo na vizazi vijavyo.

Akizungumza kwenye maadhimisho ya Siku ya Nile iliyofanyika Kijiji cha Nyashimo wilayani Magu juzi, kwa niaba ya Waziri wa Maji Dk Shukuru Kawambwa, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Dk James Msekela alisema kuwa, raia hao, wanapashwa kutumia vizuri na kuziendeleza rasilimali hizo kwa kwa manufaa yao wenyewe.

Dk Kawambwa alisisitiza kuwa, hatua hiyo itasaidia na kufanikisha maendeleo ya kiuchumi katika nchi hizo kumi zinazotegemea bonde hilo katika masuala mbalimbali ya kijamii.

Nile una rasilimali nyingi ambazo hazijatumika kikamilifu pia zipo ambazo zinawanufaisha wananchi, hivyo kuufanya mto huo, uwe endelevu unaohitaji kuhifadhiwa.

Pamoja na rasilimali nyingi kutotumika katika bonde hilo, lakini wananchi wengi wanaolizunguka ni maskini duniani, wanasumbuliwa na magonjwam hawana uhakika wa maji safi na salama kwa kunywa na matumizi ya nyumbani, pia wanakipato kidogo.

Wananchi hao, wanakabiliwa na matatizo ya umeme, ukame na hawana uhakika wa chakula kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa duniani.


Mabadiliko hayo ya hali ya hewa yanatokana na mazingira yanayotuzunguka milima, misitu, maziwa kuharibiwa huku , ardhi yenye rutuba ikipotea ,wanyamapori kupungua na uchumi kuwa dhaifu na kusababisha vijana kukosa ajira.

Wakati hayo yakitokea, idadi ya watu nayo inazidi kuongezeka, hivyo kufanya matumizi ya rasilimali nayo kuongezeka.

Tanzania inashirikiana na nchi nyingine katika umiliki, utunzaji na matumizi ya rasilimali ya maji ili kuweza kushirikiana katika kuondoa umaskini, njaa, magonjwa,uhaba wa nishati na mmomonyoko wa udongo.

Hatua hiyo ilizifanya nchi hizo, ziunde Nile Basin Inititave (NBI), kufanikisha maendeleo ya kiuchumi, kijamii kwa kuzingatia matumizi endelevu yanayozingatia usawa na faida zitokanazo na rasilimali maji ya bonde hilo.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.