Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Waomba vituo vya ARV viongezwe
Waomba vituo vya ARV viongezwe
By Habari Tanzania | Published  02/21/2007 | Habari za Kitaifa | Rating:
Na Gasper Andrew

SERIKALI imeombwa kuangalia uwezekano wa kuongeza idadi ya vituo vya kutolea huduma
ya dawa za kurefusha maisha (ARV), ili visaidie kuhudumia wagonjwa wengi zaidi wa
ukimwi mkoani Singida.

Wito huo umetolewa na Mratibu wa Mpango Kudhibiti Maambukizi ya Virusi vya Ukimwi, mkoani Singida, Dk Khalid Msangi wakati akizungumza katika warsha ya kuweka mkakati wa kupambana na ugonjwa huo.

Alisema takwimu zinaonyesha kuwa zaidi ya watu 35,000 wameambukizwa virus vya ukimwi tangu ugonjwa huo uingie mkoani Singida mwaka 1986.

Dk Msangi alisema pamoja na idadi hiyo kubwa, ni wagonjwa 1,769 tu waliojitokeza
kwenye vituo vya hospitali za Mkoa, Manyoni, Iramba, Itigi na Makiungu na kupatiwa dawa za kurefusha maisha.

Mratibu huyo alisema hali hiyo inasababishwa na idadi ndogo ya vituo na kutofikika kwa urahisi kutokana na umbali.

Kutokana na hali hiyo, Dk Msangi alisema kuna haja kwa serikali kuhakikisha kuwa
huduma hizo zinasogezwa hadi kwenye vituo vya afya na zahanati za vijijini, ili kuwafikia waathirika wengi zaidi wa ukimwi.

How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.