Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Magufuli aanza kazi baada ya matibabu Ujerumani
Magufuli aanza kazi baada ya matibabu Ujerumani
By Habari Tanzania | Published  02/21/2007 | Habari za Kitaifa | Unrated

Na Alphan Mlacha

WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, John Magufuli, amerejea kazini baada ya safari ya matibabu nchini Ujerumani na kumtetea mmiliki wa baa ya Rose Garden, iliyopo Mikocheni Dar es Salaam, akisema imejengwa kihalali kwa kufuata taratibu zote zinazotakiwa.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, waziri magufuli, ambaye alizungumzia migogoro kadhaa ya viwanja jijini Dar es Salaam, alisema mmiliki a baa hiyo anazo baraka za wizara pamoja na vibali vyote vinavyomruhusu kuendesha baa katika eneo hilo.

Alipinga madai ya Manispaa ya Kinondoni inayosema kuwa baa hiyo imejengwa katika hifadhi ya barabara. Alisema wizara yake ipo tayari kutoa vielelezo vyote vinavyothibitisha uhalali wa kiwanja hicho iwapo itatakiwa kufanya hivyo na mahakama.

Mmiliki wa baa hiyo ameingia katika mgogopro na Manispaa ya Kinondoni, inayodai kuwa eneo hilo ni eneo la hifadhi ya barabara, na ikisisitiza kuwa baab hiyo lazima ivunjwe na kuondolewa eneo hilo.

Mapema Waziri Magufuli alisema vita vyake kutetea maslahi ya wanaodhulumiwa viwanja na kuisimamia sheria ya ardhi kikamilifu ni chanzo cha baadhi ya watu kumuombea mabaya.

“Ninajua kuna baadhi ya watu wananifuatafuata kwasababu ya kusimamia kikamilifu sheria za ardhi, lakini mimi sitatetereka kamwe na ndiyo hao wanaozusha kuwa nimekufa,” alisema Magufuli.

Alisema Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi ina migogoro mingi sana na pindi migogoro hiyo inapotatuliwa na wizara yake kwa mujibu wa sheria, ndipo uhasama unapoanza kutoka kwa watu walioshindwa katika mashauri hayo.

Hii ni mara ya kwanza kwa Mgufuli kuzungumza na waandishi wa habari tangu aliporejea nchini mapema wiki iliyopita akitoka Ujerumani ambako alikuwa akipatiwa matibabue.

Akizungumzia viwanja hivyo vilivyopo katika maeneo ya Mbezi, Tegeta, Jangwani Beach na Boko, Magufuli alisema viwanja hivyo vilipimwa na kumilikishwa miaka ya 1980 hadi 1990 na vimekuwa na migogoro mingi.

Alisema wizara yake imeamua kutoa hati mpya za umiliki wa viwanja hivyo zitakazodumu kwa miaka 99 ili viweze kuwasaidia wahusika kuliko hati za sasa za umiliki wa miaka 33.

Aidha alisema migogoro ya ardhi katika maeneo hayo, inatokana na kukosekana kwa kumbukumbu au taarifa sahihi za kiofisi kuhusiana viwanja hivyo.

Aliongeza kuwa wizara imepanga kufanya uhakiki miliki za viwanja 14,531 katika maeneo ya Tegeta viwanja 5,001, Mbezi viwanja 7,149, Boko Wizara viwanja 631 na Boko Manispaa viwanja 1750.

Alisema katika maeneo hayo, viwanja vilivyoendelezwa ipasavyo ni 5,014 na ambavyo maendeleo yake ni hafifu ni 2,497.

Aliongeza kuwa viwanja 2,520 havijajulikana wenyewe ingawa tayari wameshatangaziwa wajitokeze na kutahadharisha kuwa endapo hawatajitokeza, viwanjwa hivyo vitauzwa kwa watu wengine.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.