Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Mtera hatarini kupasuka
Mtera hatarini kupasuka
By Habari Tanzania | Published  02/20/2007 | Habari za Kitaifa | Rating:
na Irene Mark

KINGO za bwawa la Mtera, ziko katika hatari ya kupasuka kutokana na kujaa maji kupita uwezo wake, kulikosababishwa na mvua nyingi zinazoendelea kunyesha.

Hali hiyo imesababisha Shirika la Umeme nchini (TANESCO), kulazimika kumwaga maji ya bwawa hilo, ili kulinusuru na hatari hiyo ya kingo kupasuka.

“Maji yatakayomwagwa ni sentimeta tisa zilizozidi, kwani tusipofanya hivyo, yanaweza kupasua kingo za bwawa na kusababisha hasara kubwa kwa taifa,” imesema taarifa ya shirika hilo iliyotolewa na Mkurugenzi Mtendaji wake, Dk. Idris Rashid.

Mkurugenzi huyo, alieleza kina cha maji kwenye bwawa hilo kimefikia mita 698.59 juu ya usawa wa bahari, kinachodaiwa kuzidi uwezo wa bwawa hilo wa kuhifadhi mita 698.50 ambacho kinahifadhi mita za ujazo milioni 3,700.

Alieleza kuwa, wastani wa maji yaliyoingia kwenye bwawa hilo kwa wiki hii ni mita za ujazo 672.87 kwa sekunde, wakati maji yanayotumika kwenye uzalishaji wa umeme ni meta za ujazo 51.10 tu.

Dk. Rashid alieleza kuwa, uongozi wa TANESCO umetoa taarifa kwa viongozi wa mikoa ya Morogoro, Iringa na Dodoma kuhusu umwagaji huo wa maji na kuwatahadharisha wakazi wa wilaya za Mpwapwa, Kilosa, Kilolo na Kilombero kutofika karibu na mito itakayokuwa na maji mengi.

Alisema, maji hayo yanaweza kuathiri madaraja, mifugo, makazi na hata kusababisha vifo vya watu kwa kuwa yatakuwa mengi na yenye nguvu.

Pamoja na umwagaji huo, TANESCO imekanusha habari za kujaa kwa tope kwenye bwawa hilo zinazozuia uzalishaji wa umeme nchini.

Uzalishaji wa umeme katika bwawa hilo ulianza Februari 8, mwaka huu baada ya kusitishwa kwa miezi minne mfululizo kutokana na kupungua kwa kina cha maji Oktoba mwaka jana. Ujenzi wa bwawa hilo ulikamilika mwaka 1981.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.