Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Cheo cha ukurugenzi BAKWATA chafutwa
Cheo cha ukurugenzi BAKWATA chafutwa
By Habari Tanzania | Published  02/17/2007 | Habari za Kitaifa | Unrated

MUFTI wa Tanzania, Sheikh Mkuu, Sheikh Issa bin Shaaban Simba, amemfuta kazi ya ukurugenzi wa dini katika Baraza la Waislamu wa Tanzania (BAKWATA), Sheikh Suleiman Gorogosi na wakurugnzi wengine wanne.

Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa juzi na Mwenyekiti wa Taifa wa BAKWATA, Sheikh Khamis Mataka, ilieleza kuwa mabadiliko hayo yametokana na mchakato wa kujipanga upya kwa ajili ya kuutumikia Uislamu.

Akitangaza mabadiliko hayo wakati wa kikao cha wakurugenzi mbalimbali wa BAKWATA, juzi, Mufti Simba, alisema ameazimia kutekeleza maoni ya Waislamu wanaolitegemea baraza hilo kwa ajili ya maendeleo yao na taifa.

Alisema kuwa, viongozi hao wataendelea kuwa wafanyakazi wa baraza, huku wakisubiri kupangiwa kazi nyingine chini ya mfumo mpya wa utendaji (MMU), wenye lengo la kuboresha huduma za baraza hilo.

Pamoja na Gorogosi, wakurugenzi wengine waliofutwa kazi na vyeo vyao kwenye mabano ni Mohamed Mvogogo (Elimu na Mafunzo ya Ufundi), Suleiman Lolila (Afya), Twaha Majaliwa (Naibu Mkurugenzi wa Dini) na Ramadhan Samamba (Usalama).

Baada ya kikao hicho, Mufti aliwaagiza wakurugenzi hao kukabidhi ofisi na majukumu yote kwa Kaimu Katibu Mkuu, Sheikh Hassan Luambano, atakayesimamia shughuli zote za kurugenzi hizo.

Aidha, katika kikao hicho, Mufti ameahidi kutangaza mfumo huo mpya (MMU) hivi karibuni na kuwashukuru wakurugenzi waliotolewa madarakani kwa ufanisi wao kwa kipindi chote walicholitumikia baraza hilo.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.