Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Mabilioni ya Kikwete yakwama
Mabilioni ya Kikwete yakwama
By Habari Tanzania | Published  02/17/2007 | Habari za Kitaifa | Unrated
na Richard Mwangulube

FEDHA za serikali zilizotengwa kwa ajili ya kusaidia ujasiriamali mkoani Arusha, bado zinaendelea kubakia katika Benki ya CRDB, zikisubiri halmashauri ya manispaa hiyo kuwasilisha orodha ya vikundi na vyama vya akiba na mikopo (SACCOS) vilivyopatiwa mafunzo.

Meneja wa CRDB Mkoa wa Arusha, Chiku Issa, alisema hadi jana benki yake ilikuwa haijapata orodha ya vikundi hivyo, jambo ambalo linaifanya ishindwe kutekeleza kwa vitendo mpango wa serikali wa kuwawezesha wananchi kiuchumi.

Benki hiyo pamoja na NMB, ndizo zimepewa dhamana ya kusimamia fedha hizo katika Mkoa wa Arusha zilizobatizwa jina la ‘Mabilioni ya Kikwete’.

Akihojiwa ofisini kwake jana, Chiku alisema, anadhani halmashauri zimeshindwa kuendesha mafunzo katika ngazi za kata na vijiji, juu ya namna ya kusimamia fedha hizo.

Alibainisha kuwa, benki hiyo hutoa mikopo hiyo kupitia SACCOS ama vikundi, kutegemea mahitaji ya chama husika, kwani fedha hizo zinahitaji uadilifu na nidhamu ya hali ya juu katika kusimamia matumizi na marejesho, ili wananchi wengine waweze kukopeshwa kupitia vikundi ama SACCOS zao.

Chiku alisema, inaelekea asasi za kifedha katika ngazi ya kata na vijiji, bado hazijawezeshwa kwa kupatiwa mafunzo ama kuelimishwa, ili wananchi ambao ni wanachama wake, waweze kukopeshwa kutoka mfuko huo wa Rais Kikwete.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.