Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Suala la ushoga latishia Waanglikana
Suala la ushoga latishia Waanglikana
By Habari Tanzania | Published  02/16/2007 | Habari za Kitaifa | Unrated

Na Simon Berege

MGAWANYIKO uliotarajiwa kujitokeza kwenye mkutano wa maaskofu wakuu wa Kanisa la Anglikana unaoendelea katika Hotel ya White Sands jijini Dar es Salaam, jana ulidhihirika baada ya maaskofu watatu waliowasilisha mada zao kutofautiana juu mwelekeo wa kanisa hilo katika suala la ushoga.

Msemaji wa mkutano huo, Askofu Mkuu wa Australia Phillip Aspinall, akizungumza na waandishi wa habari hoteli hapo baada ya mkutano wa maaskofu hao jana, alisema kuwa maaskofu watatu walitoa mada kuhusu ushoga kila mmoja akiwaonyesha msimamo tofauti na mwingine.

Alisema Askofu Robert Duncan wa Marekani alitoa mada iliyopinga kabisa uwezekano wa Kanisa hilo kukubali suala la ushoga ndani ya kanisa.

Kwa upande wake Askofu Christopher Eptino pia kutoka Marekani, alishawishi maaskofu hao kukubali mabadiliko ndani ya kanisa kwa kuwakubali mashoga.

Askofu mwingine, Bruce Mcperson pia kutoka Marekani alisema ni wakati sasa kwa kanisa kutafuta njia ya kupata suluhu ya mvutano wa suala la ushoga bila kusababisha mgawanyiko miongoni mwa wamuni wa kanisa hilo.

Maaskofu hao walihudhuria mkutano huo rasmi kwa ajali ya kuwasilisha mada zao na wanadaiwa kwamba walirejea makwao jana.

Askofu Aspinall alisema kutokana na hali hiyo maaskofu wakuu wa kanisa hilo wanatarajiwa kutoka na maamuzi ambayo hayataligwa kanisa.

Pia aliwaomba waumini wa kanisa hilo nchini kuuombea mkutano huo ili uweze kuyamaliza matatizo yote yanayolikabili kanisa.

Kanisa la Anglikana limegawanyika tangu alipotawazwa kuwa Askofu, Gene Robinson wa Marekani, na kumekuwa na shinikizo kubwa la kutaka afukuzwe kwenye kazi hiyo kwa sababu ushoga ni kinyume cha maandiko matakatifu ya Biblilia na Ukristo kwa ujumla wake.

Jana ilikuwa siku ya kwanza ya mkutano huo na baada ya mada hizo tatu za maaskofu hao, leo maskofu wakuu wanatarajiwa kujadili mada hizo kabla ya kuamua mustakabali wa kanisa hilo.

Naye mchungaji wa kanisa hilo kutoka Marekani, Caroline ambaye amekuja kuchagiza kukubalika kwa ushoga katika kanisa alisema hatma ya kanisa hilo imo mokononi mwa Askofu Mkuu wa Nigeria, Peter Akinola.

Mchungaji Caroline alimuomba Askofu Akinola kuyakubali makundi yote ndani ya kanisa ili kulinusuru lisisambaratike.

Alisema kwamba kuwakataa mashoga na hivyo kusababisha kusambaratika kwa kanisa hakutakuwa na manufaa kwa wamuni wa kanisa hilo duniani.

Maaskofu hao wakitarajiwa kuamua mustakabali wa kanisa hilo kuanzia leo, kundi la wanaharakati wa ushoga wamepiga kambi hotelini hapo wakijaribukushawishi kukubalika kwa tabia hizo ndani ya kanisa.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.