Na Abeid Poyo HIFADHI ya Wanyama ya Serengeti mkoani Mara, imepiga marufuku magari yenye uzito zaidi ya tani tatu, kutumia barabara ya Naabi mpaka Fort Ikoma inayopita ndani ya hifadhi hiyo.
Kwa mujibu wa taarifa za uongozi wa hifadhi hiyo, amri ya kuzuia magari yenye uzito mkubwa kutumia njia hiyo, inatokana na uharibifu wa barabara hiyo unaosababishwa na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha katika hifadhi hizo na maeneo ya mkoa wa Mara.
" Tunashauri magari hayo yapite barabara mbadala.....JItihada zitafanyika kurekebisha barabara hiyo mara halimya hewa itakaporuhusu ili huduma zirejeshwe tena" inasema taarifa hiyo.
Hata hivyo, taarifa inasema amri hiyo haitoyahusu magari yanayotumika kusafirisha watalii katika mbuga hiyo kubwa nchini. Uzito wa magari hayo, haukutajwa.