Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Ajali za treni, Scandnavia zaua 11
Ajali za treni, Scandnavia zaua 11
By Habari Tanzania | Published  02/15/2007 | Habari za Kitaifa | Rating:

Na Michael Uledi, Dodoma

WATU 11 wamekufa papo hapo na wengine zaidi ya 12 kujeruhiwa vibaya katika ajali mbili tofauti, ikiwamo ya kuanguka kwa treni ya abiria mkoani Kigoma.

Katika ajali ya kwanza watu wanane wamekufa wakiwamo wanafunzi wa shule ya sekondari wanne na wengine wanane kujeruhiwa baada ya basi mali ya Kampuni ya Scandinavia kugongana uso kwa uso na daladala.

Daladala hiyo mbayo kwa kiasi kikubwa ilikuwa imebeba wanafunzi wa shule mbalimbali, imepasuka upande wake wa kushoto kutokana na kishindo cha ajali hiyo iliyotokea katika Manispaa ya Dodoma eneo la Ipagala.

Miongoni mwa waliotambuliwa kuwa wamefariki dunia ni pamoja na mmiliki wa daladala hiyo, ambaye alikuwa ni dereva aliyetajwa kwa jina moja la Ali.

Wengine ni pamoja na mwanafunzi wa kidato cha pili katika Shule ya Sekondari Kisasa, Leila Ally (16), mkazi wa Kota za Reli mjini Dodoma na wanafunzi wengine watatu ambao majina yao hayajatambuliwa.

Kondakta wa daladala aliyetambuliwa kwa jina la utani la Chechu, naye alikufa papo hapo pamoja na mwanamke mmoja na mtoto anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka miwili na nusu.

Mmoja wa watu waliohusika na ubebaji wa miili ya marehemu na majeruhi kupeleka katika Hospitali ya Mkoa Dodoma, alisema daladala hilo imepasuka upande wa kushoto kutokana na kishindo.

Alisema haieleweki ajali hiyo imetokeaje kwani magari hayo yalikuwa yakipishana wakati basi la Scandinavia lilipokuwa likiingia mjini Dodoma na daladala ilikuwa inakwenda maeneo ya Ipagala.

Alisema basi la Scandinavia lilikutwa likiwa katikati ya barabara na kwamba lilikuwa limevuka kidogo mstari wa kati huku likiwa limebonyea eneo la katikati.

Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini, John Tupa, alifika katika Hospitali ya Mkoa kuona athari ya tukio hilo na Mwananchi haikuweza kuongea naye kutokana na pilikapilika za kusaidia kuokoa maisha ya majeruhi.

Naye Damas Ayuke anaripoti kutoka Kigoma kuwa watu watatu, akiwamo dereva wa treni, wamekufa baada ya treni ya abiria waliyokuwa wakisafiria kupinduka eneo la Uvinza.

Habari zilizopatikana kutoka katika eneo la tukio na kuthibitishwa na Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kigoma, Donald Ludamila, zinealeza kuwa ajali hiyo ilitokea saa 5.00 usiku wa kuamkia jana, baada ya mabehewa manne na injini kuanguka.

Ludamila alisema watu walioshuhudia ajali hiyo wanasema kuwa dereva alikufa baada ya kuruka akitaka kujiokoa, lakini mkono wake ulinaswa na injini ambayo baadaye ilimwangukia.

Waliokufa ni dereva G. Said, Asha Kigwasa na Amos Orota. Waliojeruhiwa ni Mustafa Mudangi, Hamad Rashid, Hawa Mohammed na Patrick Modaya.

Mabehewa yaliayoaguka ni daraja la kwanza na daraja la pili na kwamba idadi kamili ya watu walijeruhiwa bado haijafahamika.

Ajali hiyo ilitokea kilomita 124 kutoka Kigoma mjini na kusababisha abiria wote waliokuwa wakisafiri na treni kutoka Kigoma kwenda Dodoma kusafirishwa mabasi yaliyokodishwa Shirika la Reli Tanzania (TRC) hadi vituo vya jirani ili kuendelea na safari zao.

Treni hiyo ilikuwa na jumla ya mabehewa 11 ya abiria. Mpaka sasa matengenezo yanaendelea kwenye reli ilikotokea ajali hiyo.

Ajali hii imetokea siku chache baada ya ajali nyingine ya kuanguka kwa behewa la abiria mkoani Tabora wiki iliyopita.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.