Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  DC KASULU ANUSURIKA KUPIGWA JIWE
DC KASULU ANUSURIKA KUPIGWA JIWE
By Habari Tanzania | Published  02/14/2007 | Habari za Kitaifa | Unrated
Wazazi wilayani Kasulu wametakiwa kuhakikisha watoto wao wanaenda shule badala ya ya kuzurula mitaani na kufanya vitendo vinavyokiuka maadili ya kijamii.
 
Rai hiyo imetolewa na mkuu wa wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma Bw. Said Bwanamdogo baada ya gari lake kunusurika kuvunjwa kioo na watoto waliokuwa wakiyarushia magari katika kijiji cha Nkundutsi.
 
Bw. Said Bwanamdogo akiongea na wakazi wa kijiji hicho baada ya tukio hilo amesema ni aibu kwa mzazi mwenye mtoto mtukutu anayefanya vitendo vya hatari kwa maisha yake na jamii kwa ujumla.
 
Kwa upande wake mzee Nashon Kabarali ambaye tukio la kurushiwa mawe gari la Mkuu wa wilaya limetokea jirani na nyumbani kwake amekiri kuwepo kwa tabia hiyo baina ya watoto wanaoshinda barabarani.
 
Bw. Kabarali amesema kuwa hivi karibuni kulitokea tukio lingine kama hilo la kurushiwa mawe magari yal;iyopita katika eneo hilo na kwamba watoto wanaofanya hivyo hukimbilia porini.
 
Kufuatia hali hiyo mkuu wa wilaya ameagiza watoto hao wasakwe na kupewa adhabu ili kubadili mienendo ya tabia zao na wazazi wao pia waonywe kutokana na malezi mabovu ya watoto wao.
 
Baadhi ya madereva ambao majina yao hayakupatikana mara moja wamekiri kuwepo kwa kero katika barabara ya Kasulu Kigoma ambao huyarushia mawe magari yanayopita na kasha kukimbia

How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.