Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Norway yasifu mazungumzo ya CCM, CUF
Norway yasifu mazungumzo ya CCM, CUF
By Habari Tanzania | Published  02/14/2007 | Habari za Kitaifa | Unrated
Na Mwandishi Wetu

SERIKALI ya Norway imepongeza hatua ya Serikali ya Tanzania ya kuendeleza mazungumzo kati ya CCM na CUF na kusema yanatia moyo katika kufikia maelewano na hatimaye kuleta hali ya utulivu na amani visiwani Zanzibar.

Balozi wa Norway nchini, Jon Karleiv Andreas Lomoy, alitoa kauli hiyo jana, alipokutana na Makamu wa Rais, Dk Ali Mohamed Shein, alipokwenda kujitambulisha ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam.

Balozi Lomoy alisema Tanzania ina sifa kubwa duniani ya kudumisha amani kwa kuwa imekuwa mstari wa mbele katika kusuluhisha migogoro ya kisiasa katika nchi za maziwa makuu.

Alisema anaamini ikiwa Tanzania itafanikiwa kulimaliza suala la Zanzibar katika mazungumzo yanayoendelea sasa baina ya vyama hivyo, itaendelea kung’aa na kujijengea heshima katika jumuiya ya kimataifa.

Balozi Lomoy alimweleza Makamu wa Rais kuwa ametiwa moyo na hatua kubwa ya maendeleo ambayo Tanzania imefikia hivi sasa, ikilinganishwa na miaka ya 80 wakati alipokuwa akiishi hapa nchini.

“Niliondoka Tanzania mwaka 1988. Sasa naona kuna mabadiliko mengi tu. Hapa Dar es Salaam penyewe tu inaonyesha kuna mabadiliko makubwa,” alisema.

Balozi Lomoy alitaja nyanja za biashara, utamaduni na utafiti kuwa ni maeneo ambayo yatatiliwa mkazo katika ushirikiano baina ya Tanzania na Norway.

Katika mazungumzo hayo, Makamu wa Rais alimhakikishia balozi huyo kuwa serikali ya awamu ya nne, kupitia ilani yake ya uchaguzi 2005 – 2010, imedhamiria kuleta maendeleo ya kweli kwa wananchi wake.

Dk Shein alisema Ilani hiyo inasisitiza juu ya umuhimu wa kujenga uchumi wa kisasa na kuwawezesha wananchi kushiriki katika kujenga uchumi wa nchi yao kupitia mpango wa Mkukuta.

Aliishukuru serikali ya Norway kwa misaada yake ambayo imekuwa ikisaidia jitihada za Serikali ya Tanzania kuwaletea maendeleo wananchi wake.

Alisema uhusiano kati ya Norway na Tanzania umeendelea kuimarika, hasa baada ya utiaji saini wa makubaliano ya hivi karibuni kati ya Norway na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ya kupeleka umeme kisiwani Pemba kutoka Tanga kupitia Bahari ya Hindi.

How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.