Na Mwasu Sware
BALOZI wa Amani nchini, Paul Kimiti amesema atatumia fursa ya kushiriki kikao cha cha Kamati ya Shirikisho la Amani duniani (IFWP), kinatarajia kufanyika Korea ya Kusini wiki ijayo kujadiliana na wawekezaji wa nchini humo kwa ajili ya mradi wa mashamba makubwa ya kibiashara nchini.
Kimiti aliyasema hayo jijini Dar es Salaam juzi wakati akizungumza na Mwananchi kuhusiana na kikao hicho kinachoratarajiwa kuanza februari 20 hadi 24.
Kwa mujibu wa Kimiti, lengo ni kutaka mradi wa mashamba hayo unaotarajiwa kuwekwa Namtumbo uwe kama mfano wa kuwafundishia wakulima.
Vilevile alisema atazungumzia uboreshaji wa miundombinu, sekta za elimu, kilimo na viwanda vya usindikaji nchini.
Wengine wanaotarajiwa kuhudhuriwa mkutano huo ni marais wastaafu, maspika wa bunge na viongozi mbalimbali na kwamba hapa nchini ni pamoja na Spika wa Bunge, Samwel Sitta na mjane wa Baba wa Taifa, Mama Maria Nyerere.