Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Natafakari uamuzi wa spika’
Natafakari uamuzi wa spika’
By Habari Tanzania | Published  02/13/2007 | Habari za Kitaifa | Unrated
MBUNGE wa Mkuranga, Adam Malima (CCM) amesema kwa sasa hana haraka ya kukutanishwa na Mwenyekiti wa IPP, Reginald Mengi na badala yake atakachofanya ni kupitia upya uamuzi wa Spika, Samuel Sitta na kuutafakari.

Akizungumza na gazeti hili jana, Malima alisema kukutanishwa na Mengi siyo kipaumbele chake, ila atahakikisha anasoma tena na tena uamuzi wa Sitta aweze kujiridhisha. “Nataka nipitie tena upya uamuzi ule…nitaupitia mara 20 nitafakari halafu nitasema,”alisema Malima. Malima alisema akiupitia uamuzi huo atagundua Sitta alichomaanisha kutokana na malalamiko ya Mengi na ya kwake ambayo yote yalipelekwa katika ofisi yake. Alisema kwa sasa akisema hatamtendea haki Spika na hatajitendea haki yeye kutokana na uamuzi mrefu ambao Sitta alitumia muda mwingi kuuandaa.

Alikiri kuwa baada ya Spika kutoa uamuzi huo hajapitia tena kusoma kile kilichoandikwa. Hata hivyo hakueleza sababu ya kuamua kutopitia tena uamuzi huo ambao hitimisho lake ni upatanisho.

Gazeti hili liliwasiliana na Malima baada ya maamuzi ya Spika kuhojiwa na wananchi wengi wakitaka kufahamu mambo kadha wanayoona kama yana upungufu. Wengi wanahoji ushahidi wa kanda zilizotumika katika shauri hilo kama hazikuchezewa na pande zote kutokana na kutofautiana.

Katika suala hilo mtaalamu mmoja wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), aliliambia gazeti hili kuwa licha ya kuwa waliitwa kwenye Tume ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge, lakini hawakuhusishwa katika kuhesabu muda wa mikanda iliyowasilishwa kama ushahidi.

Mtaalamu huyo ambaye idara yake inahusika na masuala ya vipindi vinavyorushwa katika vituo vya televisheni, alisema tume yake huwa hairekodi taarifa za habari ila inachovitaka vituo hivyo ni kutunza kumbukumbu za taarifa hizo kwa miezi mitatu.

Katika uamuzi alioutoa mwishoni mwa wiki mjini Dodoma, Spika aliamua kuwasuluhisha Malima na Mengi kama njia nzuri ya kumaliza malalamiko ya watu hao wawili. Sitta alisema atawakutanisha kwa madhumuni ya kukubaliana naye utaratibu muafaka utakaojenga suluhu endelevu baina yao na kuepuka hatari ya suala hilo kushamirisha makundi yaliyochomoza ambayo yameonekana kuibua masuala ya udini, rangi na tofauti za vipato katika jamii.

How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.