Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Afrika Mashriki yatakiwa kuboresha barabara
Afrika Mashriki yatakiwa kuboresha barabara
By Habari Tanzania | Published  02/12/2007 | Habari za Kitaifa | Unrated

Na Ramadhan Semtawa

NCHI za Afrika Mashariki zimetakiwa kuimarisha miundombinu ya barabara, ili kuharakisha maendeleo ya nchi hizo.

Wito huo umetolewa kutokana na miundombinu katika baadhi ya maeneo ya nchi hizo hasa za vijijini kuwa katika hali mbaya.

Hayo yalielezwa jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Kutengeneza Matairi ya Yana, Erick Kimani, wakati wa uzinduzi wa matairi mapya na kuongeza kwamba miundombinu bora ndiyo ufumbuzi wa ukuaji wa uchumi.

Kimani alisema hivi sasa nchi za Afrika Mashariki zinazungumzia kuwa kitu kimoja, hivyo ni vema zikaangalia jinsi ya kuunganisha miundombinu bora.

Alisema kuna maeneo ya vijijini ambako kunafanyika shughuli za kilimo, lakini bado miundombinu haiko katika hali nzuri.

"Miundombinu hasa barabara nzuri ni jambo la muhimu kwa nchi zetu, matatizo ya Kenya na Uganda hayatofautiani sana na Tanzania, hivyo ni vema tukatilia mkazo suala hilo," alisema Kimani.

Kimani alisema kampuni yake itaendelea kutengeneza bidhaa zinazokidhi hali halisi ya miundombinu ya barabara iliyopo katika nchi ambazo imewekeza.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.