Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Fagio shule feki
Fagio shule feki
By Habari Tanzania | Published  06/17/2006 | Habari za Kitaifa | Unrated
Zimo zinazojiita seminari kumbe wapi
 
Na Kulwa Karedia
 
SERIKALI imetoa onyo kwa wamiliki na waendeshaji wa shule zinazojiendesha kinyume cha sheria, wakiziita seminari au za kimataifa, kumbe hazina sifa wala viwango.
 
Katibu Mkuu Kiongozi wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Ricky Mpama, alisema ofisini kwake jijini Dar es Salaam juzi kwamba, kuna watu binafsi wanaozitumia shule hizo ilhali ni batili.
 
Mpama alikuwa akitoa tamko la wizara, kutokana na kukithiri kwa shule zisizo na sifa, huku baadhi zikijipachika majina kuvutia watu, zikijionyesha kana kwamba zina hadhi ya kimataifa, kumbe hakuna chochote.
 
Alionya watu binafsi wanaotumia shule zao, wakidai kwamba ni za madhehebu ya dini (seminari), akasema tayari ujanja huo umegundulika, na ni tatizo, kwa sababu shule husika haziendeshwi kama za kidini, jambo ambalo ni kosa kwa mwenendo wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi.
 
"Hili ni kosa na ni kuinyima jamii elimu kwa kivuli cha taasisi za kidini. Wizara yangu inalifutalia suala hili na wale wote watakaobainika kukiuka kanuni na taratibu, shule zao zitaondolewa hadhi yao na kuwa shule za kawaida ili liwe fundisho kwa watu wenye tabia kama hii," alisema Mpama.
 
Alifafanua kwamba, shule za seminari husajiliwa kwa lengo la kutoa taaluma za dini kwa walengwa ambao baada ya siku zijazo watakuwa viongozi wa dini, waweze kuongeza uwezo wao wa kumudu majukumu pale wanapohitimu mafunzo yao , ili kuendelea kupanua madhehebu yao .
 
Mpama alisema kwamba, mbali ya shule hizo, pia serikali haina nia ya kugeuza shule za kawaida kuwa za kimataifa na wala haishawishi jamii kufungua shule hizo na kwamba serikali imebaini kuwa wadau wengi huanzisha shule bila kusajiliwa.
 
Katika hatua nyingine , Mpama alisema Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, imefanya mabadiliko makubwa ya mitaala ya elimu ya msingi, ikiwa ni moja ya hatua za kuboresha elimu. Hatua hizo zimekuja baada ya wadau kulalamikia utaratibu uliokuwa ukitumika.
 
Mpama alisema kwamba, miongoni mwa mabadiliko hayo ni kuanzishwa kwa somo jipya la Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) na Haiba ya Michezo pamoja na somo la Kifaransa. Mtaala wa elimu kwa shule za msingi umesitishwa hadi mwaka 2007.
 
Alisema masomo ya Kifaransa na TEHAMA yatakuwa ya hiari na yatafundishwa katika shule zenye walimu na vifaa vya kufundishia na kujifunza masomo hayo kuanzia mwakani.
 
"Kutokana na utaratibu mpya wa wizara yetu, waraka huu unaanza kutumika Januari 2007 na unafuta ule wa elimu wa mwaka 2005 na nakala zimesambazwa kwa maafisa elimu wa mikoa, maafisa elimu wa wilaya na wakaguzi wakuu wa shule wilayani," alisema Mpama.
 
Hatua hizi zinakuja wakati kukiwa na utitiri wa shule, baadhi zikiwa kwenye makazi ya watu, nyingine zikiwa hazina walimu wala vitabu, na nyingine zikiwa hazina hata majengo wala mbao za kufundishia, jambo linaloshusha kiwango cha elimu nchini. Hayo yamekuja baada ya watu binafsi kuruhusiwa kufungua shule kwa wingi.

How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.