Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Ufaransa yashtaki wachimba madini Tanzania
Ufaransa yashtaki wachimba madini Tanzania
By Habari Tanzania | Published  02/12/2007 | Habari za Kitaifa | Rating:

Na Mussa Juma, Arusha

UBALOZI wa Ufaransa nchini, umefungua kesi dhidi ya Chama cha Wachimbaji Wadogo wa Madini Mkoa wa Arusha (Arema) na Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi nchini (Tucta), ukidai kurejeshewa kompyuta na vifaa vingine vyenye thamani ya dola za Marekani 7,725,000, ambavyo ilivitoa kama mradi kwa chama hicho.

Kesi hiyo ambayo ilitajwa Februari 8, mwaka huu katika Baraza la Nyumba, mbele ya Mwenyekiti wake Hakimu, John Mgetta, Ubalozi huo unadai kompyuta hizo ambazo kwa zaidi ya mwaka sasa zimezuiliwa na kampuni ya udalali ya Mahakama ya Majembe baada ya Arema kushindwa kulipa kodi katika jengo la Tucta.

Katika Kesi hiyo, ubalozi huo unawakilishwa na wakili Elvalson Maro, wakati Arema inawakilishwa na mwenyekiti wake, Hamis Lyoba na Tucta inawakilishwa na Katibu wa Kamati ya Usimamizi wa Jengo lao mkoani hapa, Ernest Kangwa.

Kabla ya Ubalozi huo kuingilia kati, Tucta ilishinda kesi ya kudai kodi ya pango dhidi ya Arena ambao walishindwa kulipia malimbikizo ya kodi kiasi cha Sh630,000, hivyo kampuni ya Majembe kuamuriwa na mahakama kukamata mali zote za chama hicho zikiwemo kompyuta hizo.

Ubalozi wa Ufaransa ulitoa kompyuta hizo kwa mradi wa kusaidia wachimbaji wadogo ujulikanao kama Aden Project, ili kuwasaidia kutafutia masoko pia zingetumika kuendeshea mradi wa Internet, ili mradi ujiendeshe kwa faida.

Kesi hiyo imepangwa kundelea Februari 13 na 20 katika baraza hilo la nyumba mkoa wa Arusha.

Kufunguliwa kwa kesi hiyo pia kumechangiwa na mgogoro unaoendelea kufukuta ndani ya Arena baina yao huku baadhi ya viongozi wakituhumiwa kutumia mradi huo kwa manufaa yao na kutaka mradi huo uhamishie ofisi zake Mererani mkoani Manyara.

Hii ni kesi ya kwanza katika siku za hivi karibuni kwa ubalozi kwenda mahakani kudai kurejeshewa msaada walioutoa kwa taasisi hapa nchini, kutokana na kushindwa kutumika.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments
  • Comment #1 (Posted by zenno)
    Rating
    Kwanza aibu kwa kampuni kubwa kama hiyo kudai kitu kama kompyuta kwa watu masikini kama hao ambao wanategemea misaada kwa wanaojiweza.Pili kampuni hiyo ilipo kuwa ikitoa vitu hivyo ilivitoa kama msaada,na ukisha toa kitu kama msaada huna mamlaka ya kudai eti kwasababu ulitoa wewe,tayali umekwisha ita msaada hivyo wajaribu kuwa watssrabu wanaiaibisha kampuni yao.
     
Submit Comment


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.