Habari Tanzania - http://www.habaritanzania.com
Wakuu wa polisi kujadili uhalifu duniani
http://www.habaritanzania.com/articles/2897/1/Wakuu-wa-polisi-kujadili-uhalifu-duniani
By Habari Tanzania
Published on 02/10/2007
 
POLISI nchini wameandaa mkutano mkubwa wa maafisa wakuu waandamizi kujadili changamoto za uhalifu duniani.

Na Ramadhan Semtawa

POLISI nchini wameandaa mkutano mkubwa wa maafisa wakuu waandamizi kujadili changamoto za uhalifu duniani.

Mkutano huo unafanyika wakati jeshi la polisi linakabiliwa na changamoto kubwa ya kupambana na biashara ya dawa za kulevya huku likiwa limefanikiwa kwa kiasi fulani kupunguza matukio ya uhalifu mkubwa ukiwamo ujambazi.


Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, msemaji wa jeshi hilo, Esaka Mugasa, alisema mkutano huo utafunguliwa Februari 12 katika Chuo cha Polisi Moshi (CCPna Waziri wa Usalama wa Raia Bakari Mwapachu na kufungwa na Naibu wake, Mohamed Aboud Februari 16.

Mugasa, alisema changamoto za uhalifu katika karne hii ni kubwa, hivyo jeshi hilo linapaswa kuimarisha utulivu na amani kwa wananchi.

Mkutano huo utakutanisha watoa mada mbalimbali kutoka nje na ndani ya jeshi hilo.

Miongoni mwa watoa mada watakuwa ni wasomi wa chuo kikuu kutoka Kitivo cha Sheria na wadau wengine mbalimbali.

"Katika mkutano huo kutakuwa ana ubadlishanaji uzoefu, ili jeshi la polisi liweze kukabiliana na changamoto za uhalifu zinazojitokeza katika karne hii ya 21 ili kuleta utulivu na amani," alifafanua Mugasa.