Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Wilaya ya Kinondoni hakuna utawala bora
Wilaya ya Kinondoni hakuna utawala bora
By Habari Tanzania | Published  02/10/2007 | Habari za Kitaifa | Unrated

Na Simon Berege, Dodoma

HALMASHAURI ya Manispaa ya Kinondoni imeshika mkia katika utekelezaji wa vigezo vya upimaji utawala bora katika kipindi cha mwaka jana, uchambuzi uliofanywa na wataalamu wa Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) umeonyesha.

Akitangaza matokeo ya uchambuzi huo wakati akiahirisha Mkutano wa Sita wa Bunge jana, Waziri Mkuu, Edward Lowassa, alisema Manispaa hiyo ya Kinondoni ilishika nafasi ya mwisho kwa kigezo cha Uwazi na Uwajibikaji kwa kupata asilimia 43 na pia ikashika mkia katika kigezo cha Uadilifu wa viongozi na watendaji ikiwa na alama asilimia 11.

Historia inaonesha kwamba katika uchambuzi uliyofanyika mwaka 2002 Manispaa hiyo ya Kinondoni ilishika mkia katika kigezo cha uzingatiaji wa demokrasia kwa kupata alama 30 na haikufurukuta kupata nafasi ya kwanza katika kigezo chochote.

Wilaya hiyo ni maarufu jijini Dar es Salaam kwa kuwa ndipo wanapokaa viongozi wote wakuu wa kitaifa, akiwemo Rais, Waziri Mkuu, Makamu wa Rais mawaziri, mabalozi na wengine wengi ambao ni mashuhuri.

Kwa upande wa kigezo cha uwazi na uwajibikaji Wilaya ya Kilwa ndiyo iliyoongoza kwa kufanya vizuri kwa kupata asilimia 94 wakati upande wa kigezo cha uadilifu wa viongozi na watendaji zimeongoza Halmashauri za Wilaya ya Mtwara na Masasi zikiwa na asilimia 99 kila moja.

Takwimu hizo za Tamisemi zimeonesha kwamba Wilaya ya Monduli ambayo lipo jimbo la Uchaguzi la Waziri Mkuu, Edward Lowassa, imeongoza tena kwa asilimia 100 katika stadi za upangaji mipango kwa kuzingatia vigezo vya utawala bora, sawa na Wilaya za Kiteto, Simanjiro, Iringa na Mbinga.

Katika tathmini ya Mwaka 2002 takwimu zilionesha kwamba Monduli pia iliongoza kwa asilimia 100 wakati halmashauri zilizoshika mkia zilikuwa Shinyanga na miji wa Musoma zilizokuwa zimepata asilimia sifuri.

Kwa kipindi cha mwaka jana halmashauri zilizoshika nafasi ya mwisho ni Mkuranga, Bagamoyo, Kibaha na Halmashauri ya mji wa Korogwe zilizopata asilimia 70 kila moja.

Kwa upande wa kigezo cha zingatiaji demokrasia uchambuzi huo uliofanywa Juni umeonesha halmashauri zilizoongoza na asilimia zao kwenye mabano ni ya Mtwara, Mikindani na Morogoro zilizopata asilimia 95 kila moja wakati zilizofanya vibaya na asilimia zao kwenye mabano ni ya mji wa Lindi (73) na Mafia (74).

Halmashauri iliyoongoza katika kigezo cha Ushirikishwaji Jamii ni Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara (77) na Manispaa ya Temeke (76) wakati Halmashauri za mwisho zilikuwa Mafia (50) na Tandahimba ni asilimia 53. Kwa upande wa kigezo cha Utawala wa Sheria Halmashauri iliyoongoza ni Nachingwea (98) na za mwisho ni Ulanga na
pangani (50).

Kwa upande wa kigezo cha Uwazi na Uwajibikaji imeongoza Halmashauri ya Wilaya ya kilwa ikiwana asilimia 94 na ya mwisho ilikuwa Wilaya ya kiteto iliyopata asilimia 43. Halmashauri ya Manisapaa ya Morogoro mji wa Lindi imefanya vizuri zaidi kwa upande wa kigezo cha ufanisi wa utendaji kazi (72) na ya mwisho ni Tarime yenye
asilimia 41.

Waziri Mkuu alizidi kuchambua kwamba Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto imeongoza katika kigezo cha uzingatiaji wa jinsia (82) ikifuatiwa na Kahama (70) wakati za mwisho ni Wilaya ya Tunduru (10), Misungwi (12), Mbozi na Chunya zote zikiwa na asilimia 15 kila moja.

Kwa upande wa matumizi ya takwimu zilizoongoza ni Magu (93), Kilosa na Ulanga zikiwa na asilimia 90 kila moja wakati Wilaya ya Korogwe ilishika nafasi ya mwisho kwa kupata asilimia 72.

“Kwa halmashauri ambazo zimepata alama zisizoridhisha zinazo wajibu wa kuchukua hatua za haraka kuongeza juhudi za kuboresha maeneo yenye udhaifu ili kuimarisha dhana ya utawala bora” aliagiza Waziri Mkuu na kufafanua kwamba takwimu hizo zinaonesha kwamba kwa wastani halmashauri nyingi zinazingatia vigezo vya utawala
bora.

Hata hivyo, Lowassa alisema bado kuna tatizo la baadhi ya watalaam kukataa kufanya kazi katika baadhi ya halmashauri na mikoa na kutolea mfano wahasibu 192 kati ya 461 walioajiriwa katika halmahsauri 121 mwaka jana, sawa na asilimia 41.6 hawakujitokeza katika vituo vyao vya kazi walivyopangiwa.

Alisema watumishi wengine ni wakaguzi wa ndani 90 sawa na asilimia 50.3 ya
wakaguzi 179 waliyopangiwa kazi hawakujitokeza kazini vikiwemo vilivyopo mkoani Dodoma ambako kuna mawasiliano ya uhakika.

Alisema Ofisi ya Waziri Mkuu , Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Dodoma
ilitangaza nafasi 17 za wataalam wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano ya kisasa lakini ni wataalam watatu tu ndiyo waliyopatikana kwani waombaji wengi waliofanya usaili hasa wale wanaoishi Dar es salaam walieleza kutokupenda kufanya kazi Dodoma.

“Napenda kupongeza sana walimu wote nchini ambao wao wamekubali ajira katika sehemu yoyote nchini,“ alitoa pongezi hizo Lowassa na kuwataka watumishi wa fani nyingine kuiga mfano huo wa walimu.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.