Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Mahakama Dar yaelezwa polisi walivyomvuta nyeti mshtakiwa
Mahakama Dar yaelezwa polisi walivyomvuta nyeti mshtakiwa
By Habari Tanzania | Published  02/10/2007 | Habari za Kitaifa | Unrated

Na Nora Damian

MSHITAKIWA wa tano katika kesi ya wizi wa dola 2 milioni za Marekani mali ya Citi Bank. Libent Likondwa, jana aliangua kilio katika Mahakama ya Kisutu wakati akieleza madai ya kuteswa na aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Mkoa wa Dar es Salaam, Abdallah Zombe.

Mshitakiwa huyo alidai kuwa, Zombe alimtesa baada ya kukamatwa na polisi, kitendo ambacho kimechangia nguvu zake za kiume kupungua.

Akitoa ushahidi wake, alidai kuwa, Agosti 2, mwaka 2001 majira ya saa 8:00 usiku, akiwa amelala nyumbani kwake, watu 12 walikwenda kumgongea mlango, alipouliza ni kina nani, hawamkujibu.

" Baadaye walipojitambulisha kuwa ni askari na nilipowachungulia dirishani, waliponionyesha vitambulisho vyao niliwafungulia, walipoingia ndani waliniuliza kama namfahamu Kasusura , niliwajibu kuwa ni mjomba wangu, ” alidai.

Baadaye askari hao walimuuliza endapo alipewa dola 400 za Marekani na Justine Kasusura ambaye ni mshtakiwa wa kwanza katika kesi hiyo ili aweke ndani, aliwajibu hajawahi kupewa hela hizo.

Wakati akijibu swali hilo, askari mmoja alimzaba kibao na kuchukua simu yake ya mkononi, televisheni, kompyuta na Sh10,000 zilizokuwa kwenye pochi ya mkononi.

Kisha walimchukua na kumpeleka kwa Zombe, ambako aliulizwa kama alichukua fedha kutoka kwa Kasusura, baada ya kukataa, aliwaamuru wamfanyie kazi.

“ Mheshimiwa hakimu baada ya mimi kukataa, Zombe aliwaamuru vijana wake wanifanyie kazi, akawaambia wahakikishe narudi nikiwa sina miguu, ” alidai huku akibubujikwa machozi.

Askari hao walimchukua na kumwingiza kwenye gari la polisi aina ya Landrover Defender na kumlaza huku wakimkanyaga juu na kumpeleka Kituo cha Polisi Mabatini Kijitonyama, ambako aliwekwa katika chumba maalum.

Akiwa katika chumba hicho, askari hao walimfunga sponchi na pingu mikononi na kumning’iniza kwenye kenchi.

“ Wakati huo nikiwa nimening’inizwa juu, askari mmoja alichukua jiwe kubwa likiwa na kamba, akanifunga mwanzo wa korodani zangu huku wakiniuliza kama nimekabidhiwa hela na Kasusura, niliwajibu sielewi kitu chochote... nilipata maumivu makali sana, ” alidai.

Baada ya muda askari hao, walimfungua na kumrudisha tena kwa Zombe, lakini hawakumkuta, hivyo walilazimika kumrudisha rumande.

Baada ya kutoa maelezo hayo, Mwendesha Mashitaka Wakili wa Serikali, Angaza Mwaipopo, alimuuliza mshitakiwa huyo kama ana kielelezo chochote kuhusiana na kuumizwa sehemu zake za siri, alijibu hakuwa nacho.

Aliendelea kueleza kuwa, siku iliyofuata alipelekwa tena kwa Zombe na kuwaamuru askari wampeleke kwa RPC (Kamanda wa Polisi) Kituo cha Polisi Kati Dar es Salaam ambako alikutana na Kasusura.

Akiwa kituoni hapo, alidai yaliandikwa maelezo na siku iliyofuata, alipelekwa mahakamani hapo na kufunguliwa mashtaka ya kupokea vitu vya wizi na kupelekwa mahabusu katika Gereza la Segerea.

“Baada ya siku nane kwisha nilishangaa kuona Defender ya polisi walionifanyia unyama ikija pale Segerea, walinichukua peke yangu bila idhini ya mahakama kwa sababu wakati huo kesi ilikuwa tayari imekwishafunguliwa mahakamani, ” alidai.

Hata hivyo, aliyakana maelezo ambayo yaliyowasilishwa mahakamani hapo kuwa si yake kwa kuwa, wakati akihojiwa hakukuwa na mtu yeyote aliyekuwa akiandika wala mlinzi wa amani.

Alidai kutokana na maumivu aliyoyapata mikononi, alienda Hospitali ya Taifa Muhimbili MNH), lakini walikataa kumtibu na kumtaka apeleke fomu ya matibabu ya polisi (PF3) na kwamba alikwenda kituo cha polisi Magomeni ambako alipatiwa fomu hiyo na kutibiwa.

Mshtakiwa huyo alidai kuwa, daktari wa mifupa wa hospitali hiyo alimueleza kuwa mishipa ya fahamu ya mikononi imekufa na damu haizunguki vizuri. Mshitakiwa alitoa vielelezo hivyo mahakamani.

Baada ya kusikiliza pande zote, Hakimu Mkuu Mkazi Mfawidhi Sivangilwa Mwangesi, aliahirisha kesi hiyo hadi Februari 13, siku ambayo upande wa utetezi utamalizia kutoa ushahidi dhidi ya mshitakiwa wa tatu.

Kasusura wakati akitoa utetezi wake aliwahi kuileza mahakama hiyo kuwa alitaka kujinyonga kwa kutumia shati alilokuwa amelivaa mkoani Mbeya baada ya kutishiwa kupelekwa Dar es Salaam kuuonana na Zombe.

Kasusura alidai kuwa alifikia uamuzi huo baada ya askari waliomkamata mkoani humo kumtesa na kumueleza kwa kuwa alikataa kuonyesha mahali alipoficha fedha na bastola, angepelekwa kwa Zombe na huo ndio ungekuwa mwisho wa maisha yake.

Washitakiwa wengine katika kesi hiyo ni Leonard Urrasa, Wilclif Urassa , Lucy Urrasa na Libent Likondwa

Ilidaiwa kuwa, Agosti 2, 2001 katika Uwanja wa Ndege wa Mwalimu J.K Nyerere zamani Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Dar es Salaam (DIA), washtakiwa hao, waliiba dola 2 milioni za Marekani mali ya Citibank.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.