Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Mkuu wa gereza akutwa amekufa
Mkuu wa gereza akutwa amekufa
By Habari Tanzania | Published  02/9/2007 | Habari za Kitaifa | Unrated
MKUU wa Gereza la Ruanda mkoani hapa, Thobias Otto amekutwa amekufa chumbani kwake huku akiwa ameegemea stuli na mkononi akiwa na dawa ya kutibu ugonjwa wa pumu. Ofisa Mnadhimu Mkuu wa Magereza Mkoa wa Mbeya, Peter Wampandamalishi, alisema kuwa kifo cha Otto kilijulikana jana asubuhi baada ya kuchelewa kuingia ofisini.

Alisema kuwa hadi ilipofika saa mbili asubuhi, Otto alikuwa hajaripoti ofisini, hali iliyomfanya Naibu Mkuu wa Gereza la Ruanda, Fulko Mbunda kutoa taarifa kuwa alikuwa hajafika ofisini, ikizingatiwa kuwa alikuwa na tabia ya kuingia ofisini saa moja asubuhi.

Wampandamalishi alisema kuwa baada ya kupata taarifa hizo, alikwenda nyumbani kwake, akagonga mlango na alipofungua mlango kwa kutumia ufunguo wa akiba alimkuta chumbani kwake ameegemea stuli huku katika mkono wa kulia akiwa ameshika dawa ya pumu aliyoitaja kwa jina la ‘asthmatic’.

Alisema kuwa baada ya kuona hali hiyo daktari aliitwa na baada ya kumkagua, alithibitisha kuwa Kamishna huyo alikuwa amekwisha kufariki dunia. Inakisiwa kuwa alikufa kati ya saa 7 na 8 usiku wa kuamkia jana.

Otto alikuwa na historia ya matatizo ya shinikizo la damu kisukari na pumu, alisema. Otto alihamishiwa mkoani hapa akitokea Makao Makuu ya Magereza Dar es Salaam miezi sita iliyopita.

How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.