Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Waziri Chenge: TTCL si mali ya wafanyakazi
Waziri Chenge: TTCL si mali ya wafanyakazi
By Habari Tanzania | Published  02/9/2007 | Habari za Kitaifa | Unrated

SERIKALI imesema haitarajii wafanyakazi wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), kumfungia mwekezaji mpya, Saska-Tel International ya Canada kwani mwenye mali amekwisha kuamua hivyo.

“Serikali haitarajii kuona mfanyakazi ambaye maisha yake yanategemea TTCL awafungie milango wawekezaji hao. Mwenye mali kaamua kuwa anataka menejimenti ya kigeni, hawa wafanyakazi siyo mali yao,” Waziri wa Miundombinu, Andrew Chenge alisema jana mjini hapa.

Alisema Serikali haina pingamizi dhidi ya hatua hiyo ya wafanyakazi kwenda mahakamani kupinga mwekezaji huyo mpya, lakini akaahidi wizara yake itakutana na viongozi wao ili kufikia muafaka juu ya suala hilo.

Chenge alikuwa akizungumzia uamuzi wa Serikali kuipa kampuni hiyo ya kigeni menejimenti ya TTCL katika kipindi cha miaka mitatu, hali itakayosababisha wafanyakazi zaidi ya 800 kupunguzwa kazi.

Uamuzi wa kuiweka TTCL chini ya menejimenti ya kigeni ulifikiwa katika kikao cha Baraza la Mawaziri kilichofanyika mjini hapa mwishoni mwa wiki iliyopita.

SaskaTel International ilishinda zabuni iliyohusisha kampuni 12 za ndani na nje ya nchi. Chenge katika mazungumzo yake na waandishi wa habari jana hakuwa tayari kueleza bayana kiasi cha fedha kitakacholipwa manejimenti hiyo mpya ambayo itachukua nafasi za uongozi ambazo kwa sasa zinakaliwa na wazalendo.

Hata hivyo, akizungumza jana, Katibu Chama cha Wafanyakazi wa Sekta ya Mawasiliano Tanzania (TEWUTA), Yunus Ndaro alisema hatua inayowafanya kwenda mahakamani kupinga kampuni hiyo kuongoza TTCL ni kutokana na gharama kubwa ambayo TTCL itabidi ilipe.

Pia alisema wanaona kampuni hiyo ina uhusiano na Celtel International ambayo ina hisa asilimia 35 katika TTCL. Serikali inamiliki asilimia 65.

Alisema katika hesabu za haraka haraka wamegundua kuwa SaskaTel inaweza kutumia Sh bilioni 38 kwa miaka mitatu tofauti na menejimenti ya wazalendo ambayo ingetumia Sh bilioni tatu tu kwa miaka mitatu hiyo hiyo.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.