TAASISI ya kulea watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu ya J.C Foundation for Needy, inatafuta shilingi milioni 500 ili kujenga kituo cha kulelea watoto.
Akizungunza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana,Mwenyekiti wa Taasisi hiyo, Julius Makombe, alisema wameshakamilisha michoro wanachohitaji ni ufadhili.
“…katika akaunti yetu tunafedha taslimu Sh millioni 1.6 tu ambazo hazitoshelezi chochote,” alisema Makombe na kuongeza kuwa bado hawajajua walijenge wapi. Jengo hilo linatarajiwa kuwa na uwezo wa kuchukua watoto 500 au zaidi .