Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Lowassa awaita HakiElimu
Lowassa awaita HakiElimu
By Habari Tanzania | Published  02/5/2007 | Habari za Kitaifa | Rating:
na Mwandishi Wetu

SIKU tatu baada ya Rais Jakaya Kikwete kusema analifanyia kazi suala la Taasisi ya HakiElimu, Waziri Mkuu, Edward Lowassa, amewaita viongozi wa shirika hilo mjini Dodoma anakohudhuria kikao cha Bunge.

Habari kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, zimeeleza kuwa, mkutano huo wa Lowassa na viongozi wa HakiElimu, umepangwa kufanyika kesho.

Alipoulizwa na wahariri wakati alipozungumza nao Ikulu Februari mosi, iwapo kuifungia HakiElimu kutoa matangazo ni sawa na kuua nzi kwa kutumia nyundo, Rais Kikwete aliomba apatiwe muda apitie ripoti mbalimbali kabla hajatoa maelezo yake.

Swali hilo lilikuwa moja ya mwitikio wa kijamii baada ya Ofisi ya Waziri Mkuu kuizuia HakiElimu kutoa matangazo yoyote kama ilivyozoea kufanya.

Taarifa ya jana ya Ofisi ya Waziri Mkuu inasema kuwa, viongozi wa HakiElimu wamekuwa wakilalamika kuwa wanabanwa kauli katika matangazo yao kuhusu elimu ambayo yamekuwa yakionekana kuwa kinyume cha maslahi ya jamii.

Matangazo ya HakiElimu yaliwahi kupigwa marufuku mwaka 2005 kwa kauli ya Wizara ya Elimu na Utamaduni, kuwa yalikuwa kinyume cha maslahi ya jamii.

Hata hivyo, matangazo hayo, ambayo watawala wanayaona kuwa yanapuuza jitihada zinazofanywa na serikali kuboresha elimu nchini, yamekuwa yakiendelea kutokea kwenye vyombo vya habari.

Wanaharakati na wanasiasa, wameijia juu serikali kutokana na uamuzi wake wa kuizuia taasisi hiyo kutoa matangazo yake na kusema kitendo hicho kinaonyesha jinsi serikali ilivyokosa uvumilivu.

Aidha, walibainisha kuwa serikali imeonyesha ni jinsi gani isivyopenda kukosolewa pale inapotokea baadhi ya mambo kuwa hovyo.

Mwenyekiti wa NCCR–Mageuzi, James Mbatia, alisema, mtawala yeyote anayeogopa changamoto, si mwanademokrasia na pia hapendi maendeleo.

“Kutokana na matangazo yale, ni kweli walemavu na walimu wanadhalilishwa, nenda benki za NMB ujionee. Hivyo matangazo hayo ni ya kweli, yalifanyiwa utafiti. Sasa serikali inaogopa nini? Badala ya kuogopa, ifanyie kazi huo utafiti wa HakiElimu,” alisema Mbatia.

Kwa mujibu wa Mbatia, HakiElimu walitoa changamoto kwa serikali kwa kuonyesha kuwa sekta ya elimu ni dhaifu. Lakini, alisema inashangaza kuona badala ya kushughulikia changamoto hiyo, serikali imeamua kuiua HakiElimu.

Naye Mwenyekiti wa Chama cha Tanzania Labour (TLP), Augustine Mrema, alisema kipindi cha uchaguzi mkuu, wananchi walishangilia kuwa wamepata serikali bora, lakini cha ajabu inakandamiza uhuru wa kuzungumza.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.