Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Majambazi yateka mabasi, yapora abiria
Majambazi yateka mabasi, yapora abiria
By Habari Tanzania | Published  02/4/2007 | Habari za Kitaifa | Unrated
Burhani Yakub,Tanga



MABASI mawili ya Kampuni ya Hajee’s yametekwa na watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi na kisha abiria wake kuporwa, wakiwamo waandishi wa habari.

Mali iliyoporwa inakadiriwa kuwa ni fedha taslimu Sh3,982,000, simu 15 za mikononi na mali nyingine ambazo zilichukuliwa baada ya mabasi hayo kutegewa kwa magogo barabarani.

Kwa mujibu wa habari zilizoptaikana na kuthibitishwa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tanga, Issaya Mngulu ni kuwa tukio hilo lilitokea Ijumaa kati ya saa 11 na 12 jioni katika Kijiji cha Bongi Wilayani Handeni.

Waandishi wa habari waliokuwa wakisafiri na moja ya mabasi hayo, Mashaka Mhando wa Gazeti la Majira na Mashaka Kibaya wa Mwananchi waliifahamisha Mwananchi Jumapili kwa njia ya simu kuwa baada ya mabasi hayo kusimama katika eneo yalipotegwa magogo majambazi hayo yalifyatua risasi moja juu na kuwaamuru abiria kulala chini.

“Waliingia majambazi ndani ya basi tulilokuwa tumelipanda huku wakiwa na mapanga yakimeremeta na kutishia kutumaliza huku wakiamuru tulale chini, wakaanza kutupekua mifukoni abiria mmoja mmoja na wakachukua fedha na simu zetu zote,”alisema Mashaka Kibaya.

Waandishi hao walikuwa wakielekea Handeni kwa ajili ya kuhudhuria maadhinisho ya sherehe za kutimiza miaka 30 ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ambako zinafanyika kwa ngazi ya Mkoa wa Tanga walisema kuwa majambazi hao walikuwa wamejiziba usoni na nguo nyeusi.

Kamanda Mngulu alisema pamoja na fedha taslimu, simu za mikononi zilizoporwa thamani yake inakadiriwa kufikia 2,810,000 wakati vitu vingine vidogo vidogo vilivyoporwa ni vya jumla ya sh. 155,000 ambapo silaha iliyotumika kufyatulia risasi hewani ni ya aina ya bastola hata hivyo hakuna abiria aliyejeruhiwa.

Polisi wakiongozwa na Kamanda Mngulu walikuwa katika msitu unaozunguka eneo la tukio wakiwasaka majambazi hao ambao inahofiwa bado hawajatoka nje ya Wilaya ya Handeni.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.