Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Mbunge ataka uchimbaji tanzanite usitishwe
Mbunge ataka uchimbaji tanzanite usitishwe
By Habari Tanzania | Published  02/3/2007 | Habari za Kitaifa | Unrated

MBUNGE wa Same Mashariki, Anne Malecela, ameishauri serikali kusimamisha uchimbaji wa madini ya Tanzanite hadi hapo wawekezaji wa ndani watakapokuwa na uwezo wa kuyachimba madini hayo.

“Waziri Mkuu wa Malaysia aliwahi kufunga migodi yake hadi nchi ilipopata uwezo wake wenyewe wa kuyachimba. Tusipofanya hivyo, hao wawekezaji wa nje watakuwa wanayahifadhi hadi hapo yatakapokwisha ndiyo waanze kuyauza tena,” alishauri Mbunge huyo.

Kilango alikuwa akiuliza swali la nyongeza kwa Wizara ya Nishati na madini, lililotokana na swali lake la msingi alilotaka kujua mpango wa serikali katika kujitayarisha kujikomboa kwa kuchimba madini hayo bila kutegemea wawekezaji wa nje.

Akitoa majibu ya nyongeza, Waziri wa Nishati na Madini, Nadhir Karamagi alisema kwamba serikali haiwezi kufunga uzalishaji wa madini hayo wala kufukuza wawekezaji kwa kuwa itajikoseshea mapato.

Hata hivyo alisema serikali inaandaa mazingira bora ya uchimbaji wa kisasa ambao hauna athari kubwa.

Alisema kutokana na maendeleo ya teknolojia, kwa sasa upo uwezekano wa madini kuchimbwa bila kuisha ardhini, hivyo hakuna sababu ya kuhofia ikizingatiwa kwamba serikali ina mikakati madhubuti ya kuwasaidia wachimbaji wa ndani, ili waweze kunufaika na kazi wanayoifanya.

Waziri huyo pia alimhakikishia Mbunge wa Simanjro, Christopher Ole Sendeka ambayo jimbo lake ndilo linalotoa madini ya Tanzanite kwamba serikali itatoa kipaumbele kwa wachimbaji wadogo katika kugawa maeneo mapya ya migodi inayotarajiwa kufunguliwa.

Awali, Naibu Waziri wa Wizara hiyo, William Ngeleja, alisema serikali ina mkakati wa kuziandikisha kampuni za madini kwenye Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE), ili kuwawezesha watanzania wenye uwezo kumiliki migodi.

Alisema pia serikali inaandaa utaratibu wa kuwasaidia wachimbaji wadogo kupata mikopo na maarifa mapya katika fani ya uchimbaji, pamoja na kuwahimiza wenye leseni za uchimbaji madini kufanya tafiti kisha kutafuta wabia watakaoziendeleza.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.