Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Waziri ashauri wananchi kutaa misaada ya kompyuta
Waziri ashauri wananchi kutaa misaada ya kompyuta
By Habari Tanzania | Published  02/3/2007 | Habari za Kitaifa | Unrated
Na Michael Uledi, Dodoma

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Profesa Mark Mwandosya amewashauri Watanzania kukataa misaada ya kompyuta na simu za mitumba ili kuiepusha Tanzania kugeuka dampo la taka za sumu za kielektroniki.

Waziri Mwandosya alisema kuwa nchi zilizoendelea zinakuwa dampo la taka za sumu zitokanazo na vifaa hivyo vya elektroniki jambo linaloweza kuleta balaa kubwa nchini.

“Ushauri wangu ni kwamba zikataeni..., na kwa kweli tunatarajia kuweka utaratibu wa kudhibiti vifaa hivi siku za baadaye,” alisema Mwandosya.

Mwandosya aliyekuwa akijibu hoja za wabunge waliochjangia katika hoja yake ya kulitaka Bunge kuridhia Mkataba wa kuundwa kwa Kituo cha Afrika cha Usimamizi wa taka za sumu na nyinginezo.

Akizungumzia dawa ya DDT yenye mjadala mkali juu ya usalama wa matumizi yake, Mwandosya alisema tani tano za dawa hiyo zitahitajika katika wilaya 25 zenye mlipuko mkubwa wa ugonjwa wa malaria nchini.

Alisema kuwa katika wilaya hizo, DDT itatumika kudhibiti mbu na kwamba kazi hiyo litahitaji usimamizi mkubwa ili kupunguza athari zitokanazo na kemikali hizo.

Kwa mujibu wa Mwandosya, taka zenye sumu zina madhara makubwa kwa binadamu na mazingira na kwamba nyingi kati ya taka hizo zina tabia ya kuchuna vyuma na ngozi ya viumbe hai.

Tabia nyingine ya taka hizo ni kuwaka moto zenyewe katika joto la nyuzi joto 60 , kulipuka na kusababisha madhara makubwa katika muda mfupi na mrefu.

Alisema kuwa kituo hicho kitakachojengwa Afrika kusini kitakuwa na jukumu la kutoa mafunzo, teknlojia, utoaji wa habari na ushauri na kukuza uelewa wa jamii kuhusiana na usimamizi wa taka za sumu na za kawaida.

How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.