Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Michezo  »  Zanzibar zawapa kisogo Wabara
Zanzibar zawapa kisogo Wabara
By Habari Tanzania | Published  05/14/2006 | Michezo | Unrated
Zanzibar zawapa kisogo Wabara
Timu za netiboli za Zanzibar mwaka huu hazikusajili wachezaji kutoka Tanzania Bara kwa ajili ya ligi kuu itakayoanza Juni kwenye uwanja wa Gymkhana, imeelezwa.
 
Katibu Mtendaji wa Chama cha Netiboli cha Zanzibar, CHANEZA, Sharrifa Khamis ’Sherry’ alisema kwa njia ya simu mwishoni mwa wiki kuwa baada ya kupitia fomu za usajili, imebainika kuwa timu zote zimesajili wachezaji kutoka visiwani tu.
 
Sherry alisema tofauti na miaka ya nyuma ambapo wachezaji wengi wa Bara walikuwa wakikimbilia Zanzibar kusajiliwa na timu za huko, mwaka huu hakuna timu iliyochukua wachezaji kutoka upande wa pili wa Muungano.
 
’’Haieleweki kwa nini mwaka huu hakuna, ila ni mara ya kwanza kwa timu zetu kukosa wachezaji wa Bara,’’ alisema Sherry na kuongeza \”lakini ninaona sasa wameanza kuona umuhimu wa wachezaji wa visiwani kuwa nao wana uwezo mkubwa wa kucheza netiboli.’’
 
Timu za visiwani kwa wanawake ni mabingwa watetezi wa ligi kuu JKU, Polisi, Nyuki, Bandari, Mafunzo, Zimamoto, Chipukizi na Afya wakati za wanaume ni JKU, Msambweni, Nyuki na Polisi.
 
SOURCE: Lete Raha

How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.