Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »   Profesa Mukandara aweka mada kwapani kukimbia waandishi
Profesa Mukandara aweka mada kwapani kukimbia waandishi
By Habari Tanzania | Published  02/2/2007 | Habari za Kitaifa | Unrated

Na Andrew Msechu

MAKAMU Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Rwekaza Mukandara, jana aligoma kutoa mada kawenye Warsha ya Wawekezaji, akiwahofia waandishi wa habari.

Uamuzi wa Profesa Mukandara ulifuatia kushindwa kwa juhudi za takribani dakika kumi, kuwataka waandaaji wa warsha hiyo kuwaondoa wanahabari waliokuwepo kama alivyoshinikiza, ambao pia waligoma kuondoka ukumbini.

Hatua hiyo ya Profesa Mukandara iliwaacha hoi baadhi ya washiriki waliokuwa wakishuhudia mawasiliano baina ya waandishi, wawezeshaji na Profesa Mukandala, huku wakijiuliza ni kwa nini hataki waandishi wawepo.

Profesa Mukandara alitakiwa kuwasilisha mada juu ya Mtazamo wa hali ya kisiasa, sera na vyama nchini, ili kuwavutia wawekezaji hao kutoka katika nchi za Ulaya, Amerika na Afrika Kusini, waliokuwa wamekusanywa na benki ya Stanbic kwa kushirikiana na benki ya Standard ya Afrika Kusini.

Dakika chache kabla ya kukaribishwa ili kutoa mada hiyo, Profesa Mukandara, aliamua kukusanya makabrasha yake na kuondoka ukumbini saa 5:23 asubuhi, huku waandaaji wakimkimblia kumsikiliza.

Awali Profesa Mukandara aliwataka wawezeshaji wa Mkutano huo kuwatoa waandishi wa habari kwa kuwa hataki waisikilize mada hiyo.

Hata hivyo wanahabari hawakuridhika baada ya kupata ujumbe huo kupitia kwa Mwezeshaji Macocha Tembele, kuwa mtoa mada anyaefuata, ambaye ni Profesa Mukandara hayuko tayari kuzungumza wakiwepo.

"Tafadhalini, mtoa mada anayefuata hayuko tayari kutoa mada yake mkiwepo, tunawaomba mtoke mara moja akimaliza mtarejea," Tembele aliwadokeza wanahabari.

"Hili ni suala nyeti kwa jamii ya watanzania, ni vyema mkaijali pia nafasi yetu. Kwani ni suala gani ambalo anataka kuwaeleza watu hawa wa nje, ambalo watanzania hatutakiwi kulifahamu?" alihoji mmoja wa wanahabari hao.

Baada ya hapo walimshauri atoe mada hiyo huku akitumia kinga ya kitaaluma ya 'Off Record' kwa sehemu anazoona ni hatari, lakini inaonyesha kuwa hakulikubali kwani muda mfupi baadaye aliondoka.

Kuondoka kwake kulilazimisha wawezeshaji kutumia busara kuwafahamisha washiriki, kuwa kutokana na sababu zisizozuilika Mwezeshaji wa mada hiyo amelazimika kuondoka muda mfupi uliopita baada ya kupata simu ya ghafla.

"Tunasikitika, kwa bahati mbaya mwezeshaji wetu katika mada hii ya Mtazamo wa kisiasa, ameondoka ghafla baada ya kupata simu ya dharura, tutaendelea na mtoa mada anayefuata," alisema muongozaji, Rhett Groves, ambaye ni Mkuu wa Masuala ya Fedha wa Benki ya Stanbic.

Akizungumza na Mwananchi kwa njia ya simu muda mfupi baada ya tukio hilo, Profesa Mukandara alisema kwanza waandaaji hawakumfahamisha kuwa kutakuwa na vyombo vya habari awali, japokuwa hakushangaa alipovikuta katika eneo hilo.

Alisema pamoja na yote yaliyotokea, alilazimika kuondoka baada ya kupata taarifa juu ya kuandamana kwa wanafunzi.

Alisisitiza kuwa alilazimika kuacha kutoa mada hiyo mara baada ya kupata simu ya kumtaka kuwahi katika eneo lake la kazi.

"Mimi sina ugomvi na watu wa Press Waandishi), ni mwanaharakati, mwanademokrasia, ila nililazimika kuondoka kutokana na taarifa niliyopata kwa kuwa mimi ni Mkuu wa Chuo, halafu kwa kipindi hiki viongozi wa kitaifa akiwemo Waziri na Katibu Mkuu wa wizara husika, wako Bungeni, hivyo kila jambo linaniangalia mimi hapa," alisema.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
This article has been added to your 'Articles to Read' list.
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.