Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Benki CRDB yakopesha Saccos Sh27bilioni
Benki CRDB yakopesha Saccos Sh27bilioni
By Habari Tanzania | Published  02/1/2007 | Habari za Kitaifa | Unrated

Na Mwandishi wetu

VYAMA vya Kuweka na Kukopa (Saccos) vinavyopatiwa mikopo na Benki ya ya CRDB vimeongezeka kutoka 162 mwaka 2005 hadi kufikia 227 mwisho wa mwaka jana.

Benki hiyo imevikopesha shilingi 27 bilioni huku amana za vyama hivyo zikiwa zimeongezeka kutoka shilingi 1.5 bilioni mwaka 2005 bilioni hadi kufikia Sh 7 bilioni mwaka jana.

Mradi wa kutoa mikopo kwa saccos ulianzishwa na benki hiyo, mwaka 2001, kwa lengo la kutoa huduma kwa wananchi ambao hawana huduma za kibenki wanakoishi.

Taarifa ya CRDB iliyosaniwa na Mkurugenzi Mtendaji wake, Dk Charles Kimei inaeleza kuwa, vyama hivyo vimekuwa vikitoa huduma za kibenki kwa wanachama wake, hivyo kusaidia maisha ya wananchi wa maeneo vinakotoa huduma.

" CRDB hutumia wataalam hodari na wenye uzoefu mkubwa kutoa misaada ya vifaa, mafunzo na ushauri kwa saccos. Mafunzo haya huwa yanalenga mahitaji halisi ya saccos na pia huhimiza kutumika kwa usimamizi bora wa shughuli za vyama hivi," inaeleza sehemu ya taarifa hiyo.

Benki hiyo hukopesha saccos kwa riba ambayo huziwezesha kutoa mikopo kwa kwa kiwango cha riba chenye unafuu na kipato chao kuwa cha kutosha kulipa gharama za uendeshaji na kubakia na faida.

Hivi karibuni Dk Kimei alikaririwa akisema endapo wananchi watazitumia Saccos hizo vizuri, zitaweza kuboresha maisha ya wanachama wake na uchumi wa nchi.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.