Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Japan kuisamehe Tanzania deni Sh742bn
Japan kuisamehe Tanzania deni Sh742bn
By Habari Tanzania | Published  01/31/2007 | Habari za Kitaifa | Unrated

Na Jonas Songora

SERIKALI ya Tanzania na Japan, leo zinatiliana saini mkataba wa makubaliano ya kufuta deni la Sh 742 bilioni ambazo Tanzania ilikuwa inadaiwa na nchi hiyo.

Msamaha huo wa asilimia 100, una lengo la kupunguza madeni ya nje ambayo yamekuwa ni mzigo mkubwa kwa maendeleo ya uchumi.

Tanzania imeweza kufikia hatua hiyo kutokana na kutimiza masharti ya kusamehewa madeni katika mpango wa kuzisaidia nchi masikini kabisa duniani(HIPC).

Katika taarifa iliyotolewa na Ubalozi wa Japan nchini, hafla ya ya kutiliana sahihi itafanyika kwenye ofisi ya Wizara ya Fedha, ikiwakilishwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Gray Mgonja, na Balozi wake nchini, Makoto Ito kwa upande wa Japan.

Mpango huo wa kusamehe madeni unalenga kuwezesha fedha zilizosamehewa kutumika katika miradi yenye lengo la kupunguza umasikini na kuwezesha utoaji wa huduma za kijamii.

Kusamehewa kwa deni hilo kunafuatia mazungumzo aliyoyafanya Rais Jakaya Kikwete na aliyekuwa Waziri Mkuu wa Japan Kuyochiro Koyozumi, Novemba mwaka jana nchini Japan ambapo pamoja na mambo mengine aliomba kufutiwa madeni ili fedha hizo zitumike katika shughuli nyingine za kiuchumi.

Ili kutimiza azma hiyo ya kusamehe madeni,mapema mwanzoni mwa mwaka huu Makamu wa Waziri wa Fedha wa Japan Kazanori Tanaka, alitembelea nchini katika ziara ya muda mfupi kutangaza hatua iliyofikiwa na serikali ya Japan katika mpango wa kusamehe madeni.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.