Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Mashindano ya karate shuleni yaja
Mashindano ya karate shuleni yaja
By Habari Tanzania | Published  01/30/2007 | Habari za Kitaifa | Unrated
na Chase Mdoe

MASHINDANO ya karate kwa shule za msingi, sekondari na vyuo yanatarajiwa kufanyika Aprili mwaka huu jijini Dar es Salaam.

Akizungumza jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, Rais wa Chama cha Karate Tanzania (TASHOKA), Sensei Willy Ringo, alisema mashindano hayo yatawashirikisha wanafunzi watakaopenda kutoka shule za msingi, sekondari na vyuo kutoka jijini Dar es Salaam, lengo likiwa ni kuelekea kuwaunganisha na wenzao wa Kanda ya Tano Afrika.

Rais huyo aliwataka wanafunzi watakaopenda kushiriki mashindano hayo kuonana na uongozi wa TASHOKA ili kupata maelekezo zaidi.

Ringo pia alitoa wito kwa walimu watakaokuwa wakiwanoa washiriki hao, kufanya maandalizi ya kutosha kimazoezi ili kuwapa mwamko wa kuupenda mchezo huo.

“Hata walimu ambao watakuwa na jukumu la kuwafundisha wanafunzi hawa, itabidi nao tuonane kwa lengo la kupanga mikakati ya kutosha kuhusiana na maandalizi kamili ya mashindano hayo na mbinu za mazoezi zinazopaswa kufuatwa kabla ya kufanyika kwa mashindano,” alisema.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.