Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Wajenga sekondari usiku na kucha
Wajenga sekondari usiku na kucha
By Habari Tanzania | Published  01/30/2007 | Habari za Kitaifa | Rating:
Na Ally Sonda, Vunjo

MOTO uliowashwa na Waziri Mkuu, Edward Lowasa, kuhusu ujenzi wa vyumba vya madarasa na shule mpya za sekondari, umepokelewa kwa staili ya kipekee na wakazi wa Kata ya Kilema Kusini, Jimbo la Vunjo, ambapo sasa wanakesha usiku na kucha wakijenga shule yao mpya ili iweze kukamilika kabla ya Februari 28, mwaka huu.

Shule hiyo itakayokuwa na mikondo minne inajengwa kwenye kijiji cha Kilema Chini na itakapokamilika itachukua wanafunzi 160 kati ya 213 waliofaulu kwenda sekondari kutoka kwenye kata hiyo, ambao walikosa nafasi ya kujiunga kidato cha kwanza, mwezi huu.

Diwani wa kata ya Kilema Kusini, Louis Mbuya (CCM), alisema wananchi wanajitokeza kwa wingi kufanya kazi mbalimbali za ujenzi kwa kushirikiana na wakandarasi hadi usiku hali inayoonyesha kuwa watanzania wa sasa wanathamini elimu.

Mbuya aliwapongeza Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Alhaji Musa Samizi na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya hiyo, Sipora Liana, kutokana na kazi kubwa ya kutoa hamasa kwa wananchi ikiwa ni pamoja na kuwapa ujasiri wa kujitolea mali na nguvu zao katika ujenzi wa sekondari mpya na vyumba vya madarasa kwenye shule zilizopo.

“Kwa kweli Mkuu wa Wilaya na huyu mama Mkurugenzi wa Halmashauri wanafanya kazi kubwa sana jamani. Viongozi wetu wanapofanya mema, hata kama ni wajibu wao ni vizuri tuwashukuru, hivyo mimi na wananchi wa kata yangu tunawashukuru sana, wanatupa ushirikiano mzuri katika kujenga madarasa,” alisema Mbuya.

Kwa mujibu wa Diwani Mbuya, Halmashauri ya Moshi imetoa jumla ya Sh20 milioni kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vinne vya madarasa kwenye sekondari hiyo mpya.

Wiki iliyopita Mbunge wa Vunjo, Aloyce Kimaro (CCM), alizindua kampeni kabambe ya ujenzi wa vyumba vya madarasa na ujenzi wa sekondari mpya katika eneo hilo na kusisitiza kuwa ifikapo Machi 15, mwaka huu wanafunzi 1,160 sawa na asilimia 80 ya waliofaulu darasa la saba na kukosa nafasi kwenye jimbo hilo, wajiunge kidato cha kwanza.

Kwa mujibu wa Kimaro, kata nyingine ambazo zinajenga vyumba vya madarasa na idadi yake kwenye mabano ni Mwika Kusini(4), Kirua, Vunjo Magharibi (4), Marangu Magharibi (3), Kirua, Vunjo Kusini (3), Kirua, Vunjo Mashariki (3), Mamba Kaskazini (2), Makuyuni (20) na Kahe Magharibi (4).

How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.