Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Ndege yaangukia barabarani, abiria salama
Ndege yaangukia barabarani, abiria salama
By Habari Tanzania | Published  01/30/2007 | Habari za Kitaifa | Unrated

Na Hawa Mathias Mbeya

RAIA wa Afrika ya Kusini, Uingereza na Ufaransa wamenusurika kufa baada ya ndege waliyokuwa wakisafiria kutoka wilayani Chunya kuelekea jijini Dar es Salaam kuanguka barabarani.

Ndege hiyo yenye namba 5H SKY mali ya SKY AVIATIN ya jijini Dar es Salaam, ilianguka juzi katika Kijiji cha Kiwanja cha Ndege wilayani humo Mkoa wa Mbeya, muda mfupi baada ya kuruka kutoka katika Uwanja wa Ndege wa Chunya na kuharibika vibaya.

Akizungumzia ajali hiyo jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Suleiman Kova alisema kuwa ndege hiyo ambayo ilikuwa ikirushwa na rubani Yean Pierre ambaye ni raia wa Ufaransa ilikuwa imebeba abiria wawili, ambao hata hivyo hawakujeruhiwa katika ajali hiyo.

Kamanda Kova aliwataja abiria kuwa ni Jalek Dominick (49) ambaye ni raia wa Afrika Kusini na David Edwin (50) wa Uingereza ambao ni walikwenda kufanya utafiti wa udongo na miamba?wilayani Chunya.

Kwa mujibu wa Kova, uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa ndege hiyo ambayo ina uwezo wa kubeba abiria sita, ilikuwa imeruka angani umbali wa kilometa mbili kutoka ardhini na kwamba baada ya kufika angani ilipata hitilafu.

Alisema ghafla ndege hiyo ilionekana ikiteremka kwa kusererela na kuanguka katika barabara kuu ya kutokea Mbeya kwenda Chunya.
Watu walikuwamo?ndani ya ndege hiyo waliokolewa na wananchi waliofika katika eneo la tukio.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.