Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Askofu awatetea waandishi kuhusu muswada wa habari
Askofu awatetea waandishi kuhusu muswada wa habari
By Habari Tanzania | Published  01/29/2007 | Habari za Kitaifa | Rating:

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

ASKOFU wa Kanisa la Kiiinjili la Kilutheli (KKKT), Dayosisi ya Dodoma, Dk Peter Mwamasika, ameomba serikali kuzingatia mawazo ya waandishi wa habari katika utungaji wa sheria mpya ya habari.

Askofu Mwamasika alisema ni muhimu serikali iwasikilize na kuwapa nafasi wanataaluma hiyo, katika utungaji wa sheria ya uhuru wa vyombo vya habari ambayo imezua mtafaruku, kutokana na muswada wa sheria hiyo, utakaowasilishwa bungeni wakati wowote kuwa na kasoro za kitaaluma.

Askofu Dk Mwamasika alisema hayo wakati akizindua Gazeti la Dayosisi yake liitwalo Utume Mwema kwa watu wote, ambapo alisisitiza kwamba ni muhimu kwa taasisi zote kuheshimu taaluma hiyo.

Alisema serikali ihakikishwa kuwa inatunga sheria itakayolinda haki za wanahabari ili kuwapa nafasi ya kushiriki kikamilifu katika ujenzi wa taifa kwa uhuru.


“Sheria mpya ya vyombo vya habari inatakiwa kuwapa heshima wanahabari kama kipawa kinachotakiwa kutumiwa kwa uhuru, hivyo ihakikishe kuwa inalinda uhuru na haki za wanahabari kuliko watu,” alisema Askofu Dk Mwamasika

Askofu Dk Mwamasika alisema, kimsingi sheria inatakiwa kutungwa kwa ajili ya kuwapa nguvu waandishi ya kueleza ukweli.

Askofu Mwamasika aliwataka waandishi wa habari kufanya utafiti na uchunguzi wa kina katika masuala mbalimbali yatakayosaidia Tanzania na ullimwengu kwa jumla kusonga mbele.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.