Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Serikali yatafuta kampuni nyingine ya kuifyonza TTCL
Serikali yatafuta kampuni nyingine ya kuifyonza TTCL
By Habari Tanzania | Published  01/29/2007 | Habari za Kitaifa | Rating:
Na Ramadhan Semtawa

KASUMBA ya kutafuta kampuni za kimenejimenti kutoka nje kuja kuendesha makampuni ya umma nchini, ambayo imeishaingiza Serikali ya Tanzania hasara kubwa, bado iko ndani ya vichwa vya mawaziri na sasa wanatafuta mwendeshaji wa kigeni wa kukabidhiwa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL).

TTCL ambayo ni kampuni pekee ya umma ya simu za kawaida, imekuwa majeruhi wa mfumo huo baada ya baadhi ya hisa zake kuuzwa kwa kampuni ya MSI/Detecon International, ambayo iliiacha hoi baada ya mkataba wake kumalizika.

MSI/Detecon ilinunua asilimia 35 ya hisa za TTCL kwa gharama ya Sh120 bilioni, lakini ikalipa Sh60 bilioni, huku kiasi kingine kikizua mvutano mkubwa baina ya kampuni hiyo na serikali. Hata hivyo kwa mshangao wa wengi serikali iliruhusu menejimenti ya TTCL kuwa chini ya MSI/Detecon.

Baada ya mvutano wa muda mrefu na kufikisha katika mahakama ya usuluhisi ya kimataifa, waliafikiana kuwa Serikali ilipwe dola za marekani 4.5 milioni tu badala ya Dola 60 milioni ambazo walikuwa wamekubaliana awali.

Kasumba hiyo pia imeliacha hoi Shirika la Umeme nchini (Tanesco), baada ya Net Group Solutions (Pty) kumaliza mkataba wake wa kimenejimenti wa miaka minne.

Licha ya matokeo hayo, Baraza la Mawaziri linadaiwa kwamba Ijumaa ijayo litakutana mjini Dodoma, kujadili uwezekano wa kuikabidhi TTCL kwa kampuni nyingine ya kimenejimenti kutoka Canada, Saskatel International.

Taarifa zilizoifikia Mwananchi na kuthibitishwa na Waziri wa Miundombinu, Andrew Chenge, zinasema kikao hicho kitaketi kujadili kampuni ya Skaskatel International na Rites ya India, inayopaswa kuendesha Shirika la Reli nchini (TRC).

"Naomba msubiri, haya mambo yatajulikana vizuri mjini Dodoma Februari 2 na yakiwa tayari tutatoa taarifa," Chenge aliliambia Mwananchi ofisini kwake jijini Dar es Salaam wiki iliyopita.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, wakati Rites ikijiandaa kuikodi TRC, tayari kuna kila dalili kwamba huenda ikajikuta inafanya kazi katika wakati mgumu kutokana na kuwepo taarifa za tatizo ukosefu wa fedha linaloikabili kampuni hiyo.

Chenge licha ya kukiri kupata taarifa hizo, alisema tayari Serikali imetoa msimamo wake kwamba hilo haihusiki nalo kwani ni makubaliano ya mashirika hayo mawili.

Chenge alisema serikali haihusiki na mazungumzo kati ya Rites of India na kampuni yoyote itakayoingia nayo mkataba bali inasimami mkataba wa menejimenti.

"Tumeshasema hilo halituhusu, sisi tunasimamia mkataba, kama ni makubaliano ni ya kwao," alifafanua Chenge.

Wakati serikali ikisema hivyo, taarifa zaidi zilizofikia Mwananchi zinasema mshirika huyo wa Rites of India, kwa sasa yupo katika wakati mgumu kifedha unatokana na hata baadhi ya mabenki nchini kukataa kuipa mkopo.

"Hawa jamaa nasikia hata mabenki yamekataa kuwakopesha, sasa sijui watafanyaje kazi," kilidokeza chanzo kimoja.

Wakati hilo likiwa kwa upande wa TRC, TTCL, Chama cha Wafanyakazi wa Mtandao wa Simu (Tewuta) kimeanza kuonyesha msimamo wa kupinga menejimenti hiyo.

Saskatel International ilipaswa kuanza kazi ya kuendesha menejimenti ya TTCL tangu Mei mwaka jana lakini hadi sasa kumekuwa na ukimya upande wa serikali.

TTCL inaendeshwa na menejimenti ya mpito ya wazalendo tangu kumalizika mkataba wa miaka minne wa Celtel International Februari 23, 2005.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.