Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Waziri wa Afya: Hatuna ugomvi na THI
Waziri wa Afya: Hatuna ugomvi na THI
By Habari Tanzania | Published  01/28/2007 | Habari za Kitaifa | Unrated

Na Aloyce Geofrey

WIZARA ya Afya na Ustaawi wa Jamii imetoa maelezo kuhusiana na madai ya Taasisi ya Moyo nchini (THI) kuwa wizara hiyo inaikwamisha kuleta wataalamu watakaotibu wagonjwa wa moyo karibu 30.

Akitoa maelezo hayo juzi, Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Profesa David Mwakyusa, alisema kuwa wizara yake imekuwa ikishirikiana na taasisi hiyo ingawa hakusema iwapo ilijibu au haikujibu maombi ya taasisi hiyo ya moyo.

Taarifa hiyo iliyotiwa saini na Kaimu Katibu Mkuu, Dk Zacharia Berege, ilieleza kuwa Wizara ya Afya imekuwa na ushirikiano wa kutosha na taasisi hiyo, na pia ina mwakilishi katika Bodi ya Hospitali hiyo ambayo inadaiwa kutokutana kwa zaidi ya mwaka.

Dk Berege alisema kuwa Oktoba 15, 2003, Waziri wa Afya (wakati huo) akiambatana na Mkurugenzi wa THI, alitembelea Taasisi ya Magonjwa ya Moyo nchini Ujerumani ambayo ina ushirikiano na taasisi hiyo ya hapa nchini na katika mazungumzo THI ilipatiwa msaada wa dola za Kimarekani 350,000 ili kuiendeleza.

Alisema huko nyuma wizara pia ilishapeleka wataalamu kwenye taasisi hiyo tangu ikiwa na makao yake eneo la Mikocheni kwa ajili ya kufanya tathmini na kuongeza kusema timu ya kwanza ilikagua hosipitali hiyo Mei 2, 2001 na kuanisha kuwa nafasi kwa ajili ya vitengo muhimu kama maabara, Benki ya damu na chumba cha mazoezi vilikuwa finyu.

Aliendelea kusema kuwa uchunguzi ulibaini upungufu mkubwa wa watumishi, kukosekana kwa michoro "achtectural Drawings' kuonyesha jengo hilo litakavyotengenezwa kuwa hospitali. Mkurugenzi wa THI aliwaeleza kuwa vifaa walivyodai havijakaguliwa vilishakaguliwa na wataalamu wa nje kabla ya kuletwa nchini.

Pia, ilielezwa kuwa hospitali hiyo haina makubaliano yoyote ya maandishi na taasisi zinazohusiana kuleta wataalam toka nje jambo ambalo awali Masau alisema si kweli kwa kuwa tayari taasisi hiyo ilikuwa na makubaliano ya kimaandishi na taasisi za Ujerumani na Marekani.

Taarifa pia ilidai kuwa gharama za upasuaji ni kubwa kuliko za India ambapo ilieleza kuwa gharama za THI ni Sh5 hadi 6 milioni wakati India ni Sh3 hadi 5 milioni, jambo ambalo Masau aliainisha gharama za THI kuwa ni wastani wa Sh5 milioni.

Taarifa hiyo imesema kuwa Wizara inashirikiana na THI na pia inatambua mchango unaoweza kutolewa na hopitali ya Taasisi hiyo na kuwa kuna wagonjwa kadhaa wamepata tiba za operesheni ya moyo katika hospitali hiyo bila kibali.

Kuhusu ombi la THI kuiomba wizara kupeleka na kuwalipia wagonjwa wa moyo ili wafanyiwe upasuaji, wizara imekiri kusita kufanya hivyo kwa madai kuwa si vyema kufanya majaribio na afya za wananchi hasa pale serikali inapofahamu kuna uwezekano mkubwa wa mgonjwa kupoteza maisha.

Hivi karibuni wakati wa ziara ya Mama Salma Kikwete katika Taasisi hiyo, Mkurugenzi wa THI Dk. Ferdinand Masau alitoa malalamiko yake kuwa wizara inawakwamisha katika kutekeleza lengo lake la kuwasaidia watoto wenye matatizo ya moyo wapatao 200 kwa kutoandika barua ya mwaliko wa wataalam hao kama ilivyoombwa.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.