Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Sakata la mauaji ya vijana Dar lafika kwa AG
Sakata la mauaji ya vijana Dar lafika kwa AG
By Habari Tanzania | Published  01/28/2007 | Habari za Kitaifa | Unrated

Na Ramadhan Semtawa

SAKATA la mauaji ya vijana wawili yanayohusishwa na polisi, limezidi kutikisa mamlaka za serikali na tayari limekwisha fikishwa kwenye ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) kwa ajili ya kuangalia undani wa vifo hivyo.

Waziri wa Usalama wa Raia, Bakari Mwapachu, amelithibitishia Mwananchi Jumapili juzi kuhusu hatua ya suala hilo kufikishwa kwa AG.

Mwananchi Jumapili imethibitisha kwamba, ofisi ya AG ilifikishiwa jalada hilo wiki moja iliyopita.

Kwa mujibu wa chanzo cha habari cha Mwananchi Jumapili, ofisi hiyo ya AG imepelekewa suala hilo kama sehemu mpango mzima wa uchunguzi wa tume maalumu ya kuangalia undani wa sakata hilo.

Wakati sakata hilo likifikishwa kwa AG, jalada la kifo cha Hija Shaha limekabidhiwa rasmi kwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) Kamishna Robert Manumba, kwa ajili ya kufanyiwa kazi zaidi.

Chanzo cha habari cha Mwananchi Jumapili, kimethibitisha kwamba jalada hilo lilirejeshwa Jumatatu ya wiki hii kwenda kwa Manumba.

Kwa mujibu wa chanzo hicho, jalada hilo linapaswa kufanyiwa kazi kuonyesha na kueleza kwa kina kuhusu picha za mauji ambazo ziliambatanishwa kama vielelezo.

Akizungumzia suala hilo, Waziri Mwapachu, alikiri suala hilo kufika ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuangalia undani wa vifo.

" Nikweli mara ya mwisho niliambiwa suala hilo limefikishwa ofisi ya AG kwa ajili ya kuangalia Nature ya vifo vyewe," alithibitisha Mwapachu.

Waziri Mwapachu alisema kwa kuwa tayari suala hilo lipo linashughulikiwa kwa kuundiwa tume, ni lazima lifikishwe kwa Mwanasheria Mkuu.

Kwa upande wake DCI Manumba, alikiri kupokea jalada kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP), kwa ajili ya kuongeza baadhi ya mambo yaliyokesekana.

"Ni kweli jalada nimelipokea, kuna baadhi ya mambo ofisi ya DPP imeelekeza yafanyike, lakini ipo tume," alifafanua kamishna Manumba.

Uchunguzi wa Mwananchi Jumapili umebaini kwamba, hii ni mara ya pili kwa ofisi ya DPP kulirejesha jalada hilo la kifo cha Hija kwenda kwa DCI kutokana na maelezo yake kutojisholeza wakati tayari jalada jingine la Mine Chomba limekwisha rejeshwa kwa mapungufu kama hayo.

Kifo cha Hija kilitokea Januari 16, eneo la Kimara Temboni akidaiwa kuuawa na raia wenye hasira baada ya kupora gari aina ya Toyota Rav 4 kisha kumuua Mine.

Hata hivyo, utata uliopo ni kwamba Hija aliuawa akiwa katika mikono ya polisi ambao tayari walikwishamuweka katika gari lao akiwa hana hata jeraha, lakini baadaye wakaeleza ameuawa na raia wenye hasira.

Mwananchi Jumapili itaendelea kukuletea taarifa zaidi za sakata hili kadri itakavyopata habari za kina.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.