Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Balozi awatetea Net Group
Balozi awatetea Net Group
By Habari Tanzania | Published  06/15/2006 | Habari za Kitaifa | Rating:
Na James Marenga

BALOZI wa Afrika Kusini nchini, Sindiso Mfenyana, amesema wawekezaji kutoka Afrika Kusini, wamekuja hapa nchini kuokoa kampuni zilizokuwa zinakaribia kufa na si kuchuma uchumi wa nchi kama inavyodaiwa.

Mfenyana alitoa kauli hiyo juzi kwenye mkutano na waandishi wa habari, alipokuwa akizungumzia maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka 30 ya mauaji ya wanafunzi wa Soweto nchini mwake.

Akizungumza kwa tambo kuhusu wawekezaji kutoka Afrika Kusini, alidai kwamba mfumo wa mabenki hapa nchini ulikuwa unaelekea kufa na kwamba ujio wa benki za Afrika Kusini umeukomboa na sasa una hali nzuri.

Akijibu maswali aliyoulizwa juu ya watu hao wa 'Bondeni' kuchuma rasilimali za nchi na kuondoka nazo, Balozi Mfenyana alikataa katakata, akidai hakuna uhamishaji wa fedha unaofanywa na kampuni hizo kwenda Afrika Kusini kama inavyodaiwa, na kuwa zinachofanya kampuni hizo ni kuweka fedha zao kwenye mzunguko wa biashara unaonufaisha uchumi wa nchi.

"Hakuna hata senti moja iliyohamishwa na kampuni zilizoko hapa Tanzania , na hawawezi kufanya hivyo kwa sababu wanahitaji kuzizungusha kwa ajili ya kufanya biashara zaidi," alisema.

Alifikia hata kutetea Kampuni ya Net Group Solution yenye menejimenti ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), akidai kwamba hawakuwa chanzo cha matatizo mengi ya upatikanaji wa nishati hiyo hapa nchini kama inavyodaiwa.

"Net Group Solution wanadaiwa kufuja fedha zilizotokana na malipo ya umeme, lakini nataka kuwaambia kuwa hakuna hata senti moja iliyochukuliwa na kurudishwa Afrika Kusini, hawa walikuja kuitengamaza TANESCO," alidai.

Aliongeza kwamba, matatizo ya TANESCO kwa kiasi kikubwa yametokana na masuala ya ukame na uwezo mdogo wa mitambo kuzalisha umeme na hilo halingeweza kuwa tatizo la Net Group Solution.

Balozi Mfenyana ametoa kauli hiyo, wakati tayari serikali imeshasema kwamba hairidhiki na utendaji wa kampuni hiyo na imekataa kutoa muda zaidi kuiendesha TANESCO, badala yake menejitenti itawekwa chini ya wazalendo.

Kumekuwa na malalamiko mengi kutoka kwa wananchi wa kawaida, walalahoi na hata wanasiasa, juu ya kampuni za kigeni kuruhusiwa kuchuma rasilimali za nchi, kama vile madini na kupeleka kwao. Mikataba ya madini inatarajiwa kupitiwa upya hivi karibuni.

Malalamiko mengine yamekuwa juu ya mauzo ya mashirika ya umma, ikiwamo Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), iliyouzwa kwa bei ndogo, licha ya kuwa na majengo mengi yenye thamani kubwa. Sasa serikali na baadhi ya taasisi zinapanga kwenye majengo hayo na mengine yameuzwa.

Balozi huyo alisema kama kuna wananchi wanaofikiria kuwa kuna kampuni zinawanyonya, watoe taarifa zenye vielelezo kwenye ubalozi huo ili ziweze kushughulikiwa.

Sherehe za maadhimisho ya miaka 30 ya mauaji ya wanafunzi wa Soweto nchini humo zinatarajiwa kufanyika kesho, kwa tamasha litakalohusisha msanii kutoka Afrika Kusini, Nzola 7 na wasanii wa muziki wa kizazi kipya wa hapa nchini kwenye ukumbi wa Leaders Club jijini Dar es Salaam. Pia, hiyo itakuwa ni Siku ya Mtoto wa Afrika


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.