Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Kwa hili tunampongeza Waziri Margaret Sitta
Kwa hili tunampongeza Waziri Margaret Sitta
By Habari Tanzania | Published  01/27/2007 | Habari za Kitaifa | Unrated

MOJA ya mambo yanayokera katika elimu ya Tanzania, ni suala la udanganyifu wa mitihani, ambao chanzo chake ni watumishi wasio waadilifu ndani ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi inayoongozwa na Margaret Sitta.

Tatizo lingine ambalo husababisha kuwapo kwa wataalamu wasio na sifa ni suala la vyeti bandia.

Jana, Waziri Sitta, alitangaza kuwavua madaraka walimu wakuu na baadhi ya maofisa elimu wa mikoa minne ambayo imebainika kufanya udanganyifu katika mitihani ya darasa la saba mwaka jana.

Waziri Sitta, alisema tume iliyoundwa kufanya uchunguzi ilibaini kuwapo udanganyifu mkubwa kutokana na taarifa mbalimbali kuwa, watahiniwa wapatao 120 walikuwa na miandiko inayofanana.

Baadhi ya watahiniwa walipohojiwa, walikiri kwamba walikuwa wakipewa majibu ya mitihani na wasimamizi wao na wengine walisema walikuwa wakisaidiana katika kujibu maswali.

Maofisa walioathirika wanatoka katika mikoa ya Dodoma, Kilimanjaro, Shinyanga na Tabora ambayo ilitembelewa na tume maalumu ya uchunguzi kuanzia Desemba 20, mwaka jana hadi Januari 18, mwaka huu na kubaini kuwa, watumishi hao walihusika na udanganyifu wa mitihani.

Waliovuliwa madaraka ni Ofisa Elimu wa Mkoa na Ofisa Elimu wa Wilaya ya Kondoa mkoani Dodoma, wakati Ofisa Elimu wa Wilaya ya Dodoma Vijijini na Mpwapwa wamechukuliwa hatua za kinidhamu.

Katika Mkoa wa Kilimanjaro, waliovuliwa madaraka ni Ofisa Elimu Taaluma, Ofisa Elimu Vifaa na Takwimu na Ofisa Elimu ya Watu Wazima katika Wilaya ya Same.

Mkoani Shinyanga, waliovuliwa madaraka ni maofisa elimu wa wilaya za Bariadi na Kahama wakati Mkoa wa Tabora maofisa wa elimu wa wilaya za Uyui, Urambo na Nzega wamechukuliwa hatua za kisheria.

Tunapenda kuchukua nafasi hii kumpongeza Waziri Sitta kwa uamuzi huo, unaolenga kuleta heshima na hadhi ya elimu ya Tanzania.

Miaka iliyopita, tatizo la udanganyifu wa mitihani lilikuwa kubwa sana, ingawa kwa sasa limepungua kiasi.

Wapo wanafunzi waliofanya udanganyifu wakiwa darasa la saba, wapo waliofanya hivyo wakati wa kumaliza elimu ya kidato cha nne, na waliendelea kufanya udanganyifu hadi katika mitihani ya kidato cha sita na hatimaye kujikuta wakiingia Chuo Kikuu kwa udanganyifu.

Ni dhahiri kwamba, wanafunzi wa aina hiyo, wameshindwa kuleta ufanisi katika sehemu zao za kazi kwani hawakuwa na sifa ya kushika nafasi hizo.

Wapo pia wanaofanya udanganyifu kwa kununua vyeti bandia na athari zake kwa taifa ni hizo hizo za kuwa na wataalamu wasio na sifa.

Tunatoa changamoto kwa Waziri Sitta, kwamba watumishi wa aina hiyo katika wizara yako wako wengi.

Tume iliyoundwa kuchunguza uchafu huu, iendelee kuchunguza hali hiyo na watakaobainika na kuthibitisha kuhusika na udanganyifu huo, wachukuliwe hatua kali za kisheria, wasiishie kuvuliwa madaraka tu.

Wakati tunajiandaa kujiunga na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), lazima tujenga nidhamu na heshima ya elimu yetu ili tusiachwe nyuma na nchi za Kenya na Uganda.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.