Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  TPC yasimamisha uzalishaji sukari
TPC yasimamisha uzalishaji sukari
By Habari Tanzania | Published  01/26/2007 | Habari za Kitaifa | Unrated

Na Ally Sonda, Moshi

UONGOZI wa Kampuni ya Tanganyika Plant (TPC), umesimamisha uzalishaji wa sukari kwa muda usiojulikana baada ya wafanyakazi wake kugoma kwa siku mbili mfululizo.

Kampuni hiyo iliyopo katika Wilaya ya Moshi Vijijini, mkoani Kilimanjaro, inayomilika mashamba ya miwa na kiwanda cha sukari maarufu kama TPC imelazimika kusimamisha uzalishaji baada ya wafanyakazi wake zaidi ya 1,500 kugoma.

Uamuzi huo ambao unalalamikiwa na baadhi ya wafanyakazi ambao hawakushiriki katika mgomo huo uliodumu kwa zaidi ya siku mbili, uliwafurahisha walioshiriki tangu juzi.

Kutokana na hatua ya uongozi huo, wafanyakazi wote wa kampuni hiyo wamepewa likizo ya bila malipo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa juzi jioni na Afisa Mtendaji Mkuu wa TPC, Robert Baissac, idara ambazo zitaendelea kufanya kazi kutokana na unyeti wake, ni ya ulinzi na afya.

Taarifa hiyo ya maandishi imesema, wafanyakazi wa idara nyingine nyeti wataitwa watakapohitajika, ikiwa ni pamoja na wafanyakazi waandamizi ambao watakuwapo kazini kama kawaida.

Baissac alifafanua kuwa kampuni imefikia hatua hiyo baada ya kushauriana na vyombo vya serikali ili kuokoa maisha ya wafanyakazi na mali za kampuni, kutokana na vitisho vinavyotolewa na baadhi ya wafanyakazi, vya kutaka kuwadhuru baadhi ya maofisa na kuhujumu kiwanda na mali zake.

Alisema mgomo huo ulioanza Januari 23, mwaka huu, unaongozwa na kikundi kidogo cha wafanyakazi, ambao huwashinikiza na kuwalazimisha wengine waadilifu wasiingie kazini.

Aliwaomba wafanyakazi wote kuendelea kubaki majumbani mwao kwa utulivu na usalama na amani katika kipindi chote ambacho uongozi huo ukishirikiana na mamlaka nyingine kuupatia ufumbuzi wa mgogoro huo.

Wafanyakazi wa TPC, wamegoma kufuatia malalamiko waliotoa juzi mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Alhaji Mussa Samizi kwamba wamekuwa wakinyanyaswa na mwajiri wao bila sababu yoyote.

Miongozi mwa manyanyaso hayo ni pamoja na kulazimishwa kuendelea kukatwa kwa asilimia 2 ya mishahara yao kuchangia Chama Cha Wafanyakazi wa Mashambani na Kilimo (TPAWU) wakati wao hawakitaki.

Shinikizo lingine la mgomo huo ni kutaka wafanyakazi wenzao wanne waliosimamishwa kazi kutokana na kuhojiwa na kituo kimoja cha televisheni nchini, warejeshwe kazini bila masharti na kuitaka kampuni iheshimu mkataba wa kazi, ambao walidai kwamba umekuwa ukikiukwa na baadhi ya vifungu na vingine kubadilishwa kwa maslahi ya mwajiri.

Walisema kwa hivi sasa hawana haja ya kumsikiliza kiongozi mwingine yeyote wa Serikali kuhusu mgogoro wao na mwajiri huyo, isipokuwa Rais Jakaya Kikwete na Waziri Mkuu, Edward Lowasa ambao wanaamini wataweza kumaliza tatizo hilo.

Baadhi ya wafanyakazi hao waliogoma, Jumanne iliyopita walimshambulia kwa mawe na ngumi Afisa Mtendaji Utawala, Jaffar Ally na kumjeruhi sehemu ya juu ya jicho la kulia.

Baada ya Samizi kukutana na wafanyakazi hao kuwasihi warejee kazini bila ya mafanikio, alisema wanayo hiyari ya kuwacha kazi na kuomba mafao yao au kuendelea na kazi wakati serikali na uongozi wa Kampuni unafanyia kazi malalamiko yao.

Shughuli za Kampuni hiyo zimesimamishwa ikiwa ni pamoja na kuzimwa kwa Kiwanda cha Sukari na wakati huo huo askari Polisi wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) wamepelekwa kiwandani hapo kupambana na tukio lolote litakalotokea.
 


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.