Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Waziri: Polisi Zanzibar wadhalilisha wanawake
Waziri: Polisi Zanzibar wadhalilisha wanawake
By Habari Tanzania | Published  01/25/2007 | Habari za Kitaifa | Unrated
na Mwandishi Wetu

WAZIRI wa Kazi, Maendeleo ya Vijana, Wanawake na Watoto, Asha Abdalla Juma, amelieleza Baraza la Wawakilishi Zanzibar kuwa polisi wamekuwa miongoni mwa makundi ya watu yanayoongoza katika kuwadhalilisha wanawake na watoto Zanzibar.

Asha ambaye alikuwa akijibu swali la Mwakilishi wa Mfenesini, Ali Abdalla Ali (CCM), alisema hadi kufikia Desemba mwaka jana, kesi za unyanyasaji wanawake na watoto zimeongezeka na kufikia 147.

Waziri huyo aliwalaumu polisi hao kwa kuwapa mimba wasichana, ikiwa ni pamoja na kuwatorosha makwao bila ya kupata baraka za wazazi wao.

Alisema hadi sasa ofisi yake ina kesi tatu za askari polisi waliolalamikiwa kuhusika na unyanyasaji wa wanawake na watoto.

Waziri huyo alisema, hata baada ya taarifa kutolewa, wakuu wa jeshi hilo wameshindwa kutoa ushirikiano wowote na serikali.

Aliwaeleza wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kwamba yeye binafsi alichukua hatua ya kuwaita askari hao, lakini hawakuitikia wito na kulazimika kuwasiliana na mabosi wao, lakini nao hadi sasa hawajajitokeza.

“Baadhi ya askari tunakiri kwamba wanachangia katika matatizo haya kwa kutotoa msaada ulio sahihi kwa waathirika,” alisema Waziri Asha.

Alieleza kwamba, kutokana na ukubwa wa tatizo hilo, wizara hiyo imeamua kukutana na watendaji wa Polisi, Wizara ya Afya na wakurugenzi wa mashitaka Zanzibar kupanga mikakati ya pamoja kumaliza tatizo hilo.

“Ni kweli wapo baadhi ya askari ambao wamekuwa wakijishirikisha na vitendo vya unyanyasaji kwa wanawake na watoto na wamekuwa wakaidi wanapoitwa kwa mashauriano, wao na mabosi wao,” alilalamika Waziri Asha.

Alieleza kwamba, kutokana na vikwazo vinavyojitokeza, hadi sasa hakuna askari aliyechukuliwa hatua na akaahidi kwamba hata hivyo wizara yake itaendelea kupiga vita unyanyasaji.

Waziri huyo alisema hadi sasa zipo kesi za makundi manne, ikiwamo ya wanawake kunyimwa huduma, kunyang’anywa mali, kubakwa na vitendo vya kupachikwa mimba nje ya ndoa.

Hata hivyo alisema kwamba viongozi wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wanastahili kupongezwa kutokana na mashirikiano wanayoyatoa sambamba na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kaskazini Unguja, ambaye naye ameonyesha juhudi za kupiga vita unyanyasaji.

Hivi karibuni, Waziri Asha alisema kwamba, kulijitokeza tabia ya baadhi ya watoto kutelekezwa katika ofisi yake na wengine kupelekewa nyumbani, baada ya wazazi wao kutofautiana katika familia.

Muda mfupi baada ya Waziri Asha kumaliza kujibu swali hilo, alionekana Kamishna wa Polisi Zanzibar, Khalid Idd Nuizani, katika viwanja vya Baraza la Wawakilishi.

Kamishna huyo aliingia moja kwa moja katika chumba cha kupumzikia wageni, lakini hata hivyo haikueleweka mara moja madhumuni ya ujio wake.

Kwa mujibu wa sheria za mwenedo wa makosa ya jinai Zanzibar, mtu yeyote anayepatikana na hatia katika makosa ya ubakaji, kumpachika mimba msichana au kumtorosha, adhabu yake ni miaka 30 jela.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.