Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Mafao ya majaji kupanda
Mafao ya majaji kupanda
By Habari Tanzania | Published  01/25/2007 | Habari za Kitaifa | Unrated
na Irene Mark

WAKATI ripoti ya tume iliyoangalia mishahara ya watumnishi wa umma ikiwa inasubiri kufanyiwa kazi na Rais Jakaya Kikwete, Bunge limepanga kujadili muswada wa kuongeza mishahara na masilahi ya majaji nchini, katika mkutano wake wa sita unaotarajiwa kuanza wiki ijayo.

Masilahi duni ya watumishi wa Idara ya Mahakama nchini, inatajwa kuwa moja ya mambo yanayoendeleza rushwa katika idara hiyo nyeti katika kutoa haki.

Aidha, hatua hiyo inakuja siku chache tu baada ya Rais Kikwete kuvunja rekodi kwa kuwateua kwa mpigo majaji 20 wa Mahakama Kuu na siku chache baadaye akasema uamuzi huo ulikuwa ukilenga kuimarishwa kwa idara hiyo ambayo imekuwa ikikabiliwa na matatizo mengi.

Taarifa iliyotolewa jana na Katibu wa Bunge, Damian Foka, ilisema kuwa, mbali na muswada huo utakaoleta neema kwa majaji, Bunge pia litajadili miswada mingine saba, ukiwamo muswada wa Chuo cha Sheria (The Law School of Tanzania bill) na muswada wa sheria ya bahari kuu kama ilivyorekebishwa mwaka jana.

Kwa mujibu wa Foka, jumla ya miswada minane ya sheria ya serikali itajadiliwa na maazimio manne yatawasilishwa ili kuridhiwa katika kikao hicho kilichopangwa kuanza Januari 30 na kumalizika Februari 16, mwaka huu.

Miswada mingine itakayojadiliwa ni wa Sheria ya Usajili wa Biashara wa mwaka 2006 na muswada wa sheria ya kufanya marekebisho ya sheria mbalimbali.

Pamoja na miswada hiyo, Bunge pia litajadili kuhusu Muswada wa Sheria ya kuweka mwongozo wa kuandaa, kuendesha na kutekeleza sheria ya mipango ya ardhi ya mwaka jana.

Bunge pia litajadili Muswada wa Sheria ya Kuanzisha Bodi ya Usajili ya Mipango Miji ya mwaka jana na sheria ya kuweka uongozi wa kuandaa na kutekeleza masuala yahusuyo mipango miji.

Aidha, mkutano huo utaridhia mkataba wa Shirika la Afya Duniani kuhusu udhibiti wa bidhaa za tumbaku wa mwaka 2004 na mkataba wa kuundwa kwa kituo cha Afrika cha usimamizi wa taka za sumu na nyinginezo.

Suala hilo la tumbaku linakuja siku chache tu baada ya wajumbe wa kamati ya Bunge kupendekeza kupigwa marufuku kilimo cha zao hilo.

Azimio jingine litakaloridhiwa kwenye mkutano huo ni azimio la marekebisho ya mkataba wa kuanzishwa kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki la mwaka jana, na mkataba wa Afrika wa Haki za Binadamu na watu kuhusu haki za wanawake.

Katika mkutano huo, ripoti za kamati tisa za Bunge na hoja binafsi ya Mbunge wa Geita, Ernest Mabina (CCM) ya kutaka Kampuni ya uchimbaji wa dhahabu ya Geita (GGM) kuwalipa fidia wananchi wanaozunguka mgodi huo itajadiliwa.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.