Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Tuhuma za rushwa zainyemelea Temeke
Tuhuma za rushwa zainyemelea Temeke
By Habari Tanzania | Published  01/23/2007 | Habari za Kitaifa | Unrated
na Mwandishi Wetu

BAADHI ya watendaji katika Manispaa ya Temeke, wamejiingiza katika kitendawili kigumu baada ya kushidwa kuwasilisha nyaraka maalumu za gari la zimamoto (Manufactural Warrant) katika Wizara ya Miundombinu ili kupata usajili kama ilivyoelekezwa na wizara.

Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili na kuthibitishwa na vyanzo vyetu katika Wizara ya Miundombinu, umebaini kuwa watendaji wa manispaa hiyo wameshindwa kuwasilisha nyaraka hizo na inaaminika kuwa hazipo.

Hata hivyo, inaelekea kuwa gari hili si jipya kama ilivyodaiwa na manispaa hiyo kwani imeshindwa kuwasilisha nyaraka hizo. Iwapo itathibitika kuwa gari hili si jipya, ni dhahiri kuwa baadhi ya watumishi wa manispaa hiyo watatakiwa kutoa maelezo ni kwa nini walidanganya kuwa gari hilo ni jipya.

Aidha, watatakiwa watoe maelezo ya kina kwa nini wametumia fedha nyingi kununua gari lililotumika, fedha ambazo zingetosha kununulia gari jipya.

Habari zilizopatikana zinaeleza kuwa siku moja baada ya gazeti hili kuripoti kwa mara ya kwanza sakata hilo, watendaji kutoka manispaa hiyo waliwasilisha nyaraka za mkataba wa ununuzi wa gari, nyaraka ambazo hakizuhitajika wizarani.

Nyaraka hizo za mkataba wa ununuzi zenye kurasa mbili, ziliwasilishwa na watendaji wa manispaa wakiwamo Mwanasheria na Ofisa Usafirishaji siku ya Januari 12.

Hata hivyo, maofisa wa wizara walizikataa nyaraka hizo kwa kuwa si ambazo wanazihitaji ili kusajili gari hilo.

“Nyaraka hizo za mkataba wa ununuzi hazitoshi na wala haziwezi kuthibitisha kuwa gari ni jipya, nashindwa kufahamu tatizo liko wapi kwani ‘Manufactural Warrant’ ni nyaraka ambayo huwa inaambatanishwa na nyaraka nyingine.

“Na kama kweli ni jipya ina maana wanashindwa kuwasiliana na kampuni husika ili kuipata nyaraka hiyo? Ninaamini kuwa kama wangefanya hivyo wangeletewa nyaraka hiyo haraka, lakini kwa muda ambao wamekuwa wakiitafuta, inatia wasiwasi kwani si manispaa ya kwanza kutuyumbisha na magari yenye utata,” kilieleza chanzo hicho.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.