Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Mhadhiri ahofu Tanzania kushambuliwa na Marekani
Mhadhiri ahofu Tanzania kushambuliwa na Marekani
By Habari Tanzania | Published  01/22/2007 | Habari za Kitaifa | Unrated

Na Muhibu Said

BAADHI ya wahadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), wameonya kuwa mashambulizi ya Marekani dhidi ya Somalia hivi karibuni, yatakuja pia Tanzania kwa kuwa nchi hiyo inaamini kwamba wafuasi wa mtandao wa kigaidi wa Al-Qaeda wapo pia hapa nchini.

Wameyasema hayo siku chache baada ya ndege za kivita za Marekani zilizoruka kutoka kwenye meli za kivita, kushambulia Somalia kwa makombora na kuua watu kadhaa na kujeruhi wengine katika kile kilichoelezwa kuwa ni kusaka wafuasi wa mtandao wa Al-Qaeda nchini humo.

Akizungumza katika mhadhara wa kujadili kilichotokea na kinachoendelea kutoka Somalia, katika ukumbi wa Starlight, jijini Dar es Salaam, Ijumaa ya wiki iliyopita, Profesa Hamza Njozi, alisema sheria ya ugaidi iliyotungwa na serikali kwa shinikizo la Marekani, ni uthibitisho wa dhana ya kuwapo magaidi Tanzania ambao ndio walengwa wakubwa wa mashambulizi ya nchi hiyo duniani.

Profesa Njozi, alisema uthibitisho mwingine ni kauli ya mtaalam mmoja wa masuala ya ugaidi duniani ambaye katika moja ya maandiko yake alikanusha kuwapo kwa wafuasi wa Al-Qaeda Tanzania, lakini akadai kwamba waliopo ni mashabiki wa mtandao huo.

Kutokana na hali hiyo, Profesa Njozi alisema kwa kuwa operesheni za Marekani za kuwasaka Al-Qaeda, zimekwisha kuingia katika Ukanda wa Afrika Mashariki na kutumia nchi kama vile Djibouti kama kituo chake cha kijeshi kwa ajili ya kuendesha operesheni hizo na kutahadharisha kwamba baada ya mashambulizi dhidi ya Somalia, wakati wowote yatakuja pia Tanzania.

Hivyo, alisema hakubaliani na agizo lililotolewa hivi karibuni na Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai nchini (DCI), Robert Manumba, la kuwataka Watanzania kutojihusisha na operesheni za Marekani nchini Iraq kwa kuwa mambo hayo yanafanyikia mbali na Tanzania.

"Tusifikiri mashambulizi ya Somalia hayatuhusu Watanzania, wakimaliza Somalia watakuja pia Tanzania, Marekani imekwisha kusema na hapa Tanzania Ma-Al-Qaeda wapo pia na ndio maana imetungwa sheria ya ugaidi na yupo mtaalam wa masuala ya ugaidi aliyesema Tanzania hakuna Ma-Al-Qaeda, lakini kuna mashabiki wa Al-Qaeda," alisema Profesa Njozi.

Hata hivyo, aliwapongeza Watanzania kwa kutokutetereka licha ya Marekani kuzishambulia kwa nyakati tofauti nchi za Afghanistan, Iraq, Sudan na Somalia.

Akichangia mjadala huo, Profesa Haroub Othman, alisema njia pekee ya kuisaidia Somalia, si kupeleka majeshi ya kulinda amani, badala yake ni kuisadia kuunda serikali ya kitaifa inayoungwa mkono na wananchi wote na kuleta maelewano baina yao.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.