Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Mahujaji kuwasili kesho kutwa
Mahujaji kuwasili kesho kutwa
By Habari Tanzania | Published  01/18/2007 | Habari za Kitaifa | Rating:

Na Muhibu Said

MAHUJAJI 277 wakiwamo maofisa watano waandamizi wa Baraza Kuu la Waislamu wa Tanzania (Bakwata) waliomaliza ibada ya hijja nchini Saud Arabia mwishoni mwa mwaka jana wanatarajiwa kuwasili nchini kesho kutwa.

Mahujaji hao wanaoongozwa na Mufti wa Tanzania, Sheikh Mkuu, Issa bin Shaaban Simba, walisafirishwa na Bakwata na taasisi za Taibah na Tanzania Muslim Hajj Trust.

Akizungumza na Mwananchi kwa njia ya simu kutoka Saudi Arabia jana, Katibu wa Kamati ya Umra na Hijja ya Bakwata, Alhaj Imam Swedi Swaibu, alisema mahujaji hao wanatarajiwa kuingia nchini kwa ndege ya Shirika la Ndege la Yemenia saa 10:00 alfajiri kesho kutwa.

Alhaj Swedi, alisema hadi kufikia jana walikuwa bado wako mjini Madina, Saudi Arabia, wakiendelea kutekeleza baadhi ya ibada, ikiwa ni pamoja na kutembelea maeneo mbalimbali matukufu na ya kihistoria ya dini ya Kiislamu yaliyoko mjini humo.

"Tuko ziarani Madina, tunatembelea maeneo ya kihistoria na matukufu na kumaliza siku tisa za swala arubaini," alisema Alhaj Swedi.

Zaidi ya mahujaji 2,000 kutoka Tanzania Bara na Zanzibar, walishiriki ibada ya Hijja, mwaka huu, nchini humo na baadhi yao, walianza kurejea nchini wiki iliyopita. Mahujaji wa Zanzibar, walisafirishwa na taasisi ya Istiqama iliyoko chini ya Idara ya Wakfu na Amana ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ).


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.